Ukraine imelengwa leo Jumamosi asubuhi, Februari 7, na shambulio kubwa kwenye gridi yake ya nishati, na kusababisha kukatika kwa umeme katika sehemu kubwa ya nchi, shirika la umeme la Ukraine, Ukrenergo, limetangaza, likinukuliwa na shirika la habari la AFP. “Urusi inafanya shambulio lingine kubwa dhidi ya vituo vya gridi ya umeme vya Ukraine.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shambulio kubwa la Urusi kwenye gridi ya umeme ya Ukraine limesababisha kukatika kwa umeme kote nchini Jumamosi asubuhi, kampuni ya umeme ya Ukraine ilitangaza. Urusi imekuwa ikifanya operesheni ya mashambulizi dhidi ya gridi ya umeme ya Ukraine kwa miezi kadhaa, na kusababisha mgogoro mbaya zaidi katika sekta hiyo tangu kuanza kwa mashambulizi hayo mwaka wa 2022.

Kutokana na uharibifu uliosababishwa na adui, kukatika kwa umeme kwa dharura kumetekelezwa katika maeneo mengi,” Ukrenergo imesema kwenye Telegram, huku jeshi la Poland likitangaza kuwa limetuma ndege kulinda anga yake, kama ilivyo kawaida katika tukio la mabomu ya Urusi yanayolenga magharibi mwa Ukraine.

Mamia ya maelfu ya nyumba hujikuta gizani mara kwa mara na halijoto ya baridi kali.

leo Jumamosi asubuhi, mamlaka mjini Kyiv zimeripoti kukatika kwa umeme, mji ambao uliathiriwa sana katika wiki za hivi karibuni.

Halijoto ilishuka hadi -5°C katika mji mkuu mapema asubuhi na inatarajiwa kushuka zaidi mwishoni mwa wiki hii, na kufikia chini hadi -20°C siku ya Jumatatu. Milipuko na kukatika kwa umeme pia vimeripotiwa magharibi.

Mashambulizi haya mapya yanakuja siku moja baada ya mashambulizi huko Moscow yaliyomjeruhi afisa mkuu wa idara ya ujasusi katika jeshi la Urusi, Jenerali Vladimir Alekseyev.

Mamlaka ya Urusi ilihusisha Kyiv kwa shambulio hilo, ambayo haijazungmza chochote.

Hayo yanajiri wakati wajumbe wa Urusi na wale wa Ukraine walikutana Abu Dhabi siku ya Jumatano na Alhamisi, mbele ya wawakilishi wa Marekani, kujadili njia ya kuondokana na karibu miaka minne ya vita nchini Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *