Zaidi ya bilioni 33.6 zinataraji kutumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika halmashauri ya mji wa makambako ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali, ulipaji mishahara pamoja na kuwezesha makundi maalumu ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Fedha hizo ni fedha ambazo zinataraji kukusanywa kwa mwaka wa fedha 2026/27 katika mgawanyo ufuatao. Mapato ya ndani ni zaidi ya bilioni 5.3, fedha kutoka serikali kuu Bil.27.3 na fedha za wahisani kutoka nnje ni Bil.2.9.

Baadhi ya Madiwani wa halmashauri ya mji makambako akiwemo Hanana Mfikwa wamesema rasimu hii ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 26/27 itakuwa na matokeo chanya na imejibu mahitaji ya wananchi kutokana na kugusa maeneo muhimu hasa eneo la Afya.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa walioshiriki katika kikao hiki cha ushauri wa maendeleo ya wilaya DCC, wanasema bajeti hii iliyopitishwa inapaswa kuzingatia hasa mahitaji ya wananchi hususani maeneo nyeti Kama AFYA mathalani upatikanaji wa dawa Hospitalini, vituo vya afya na zahanati.

Kwa kauli moja wajumbe wa kikao hiki wameridhia na kupitisha zaidi ya bilioni 33.6 kuwa bajeti ya fedha ya halmashauri ya mji makambako kwa mwaka wa fedha 2026/27.

#RFAOnline
#HabariStartv
@dkhan1410
MWISHO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *