‎#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limemkamata fundi magari mkazi wa Makambako, Bashiru Madembwe, kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa gari kwa kutumia silaha katika mji wa Tunduma.

Tukio hilo lilitokea Disemba 16, 2025 majira ya saa sita usiku, ambapo mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake wanadaiwa kumtishia kwa bastola ya kienyeji Bwana Jovin Kafana na kumnyang’anya gari lake aina ya Mitsubishi Outlander lenye namba za usajili T.897 EAC.

Baada ya msako mkali uliofanywa na jeshi la polisi, gari hilo lilifanikiwa kupatikana likiwa limefichwa kwenye shamba la mahindi katika Kijiji cha Iyai, wilayani Mufindi, mkoani Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, SACP Augustino Senga, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kupatikana kwa gari hilo, akibainisha kuwa ushirikiano wa kiintelijensia umeendelea kuzaa matunda katika kukabiliana na uhalifu wa kutumia silaha.

Kufuatia mfululizo wa matukio ya uhalifu katika mji wa Tunduma, Kamanda Senga ametoa onyo kali kwa wahalifu na kusisitiza kuwa jeshi hilo limejipanga vyema kuimarisha ulinzi na usalama.

Baadhi ya wananchi wametoa maoni mseto kuhusu hali ya usalama mkoani humo, huku wakiliomba jeshi la polisi kuongeza doria maeneo ya mipakani ili kudhibiti matukio ya wizi wa vyombo vya moto yanayochipuka kwa kasi.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *