#HABARI: Zaidi ya nyumba 80, vyumba vinne vya madarasa, na makanisa katika Kata za Mabalanga na Jaila, wilayani Kilindi, mkoani Tanga zimeezuliwa na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali.
Maafa hayo yamesababisha baadhi ya wananchi kukosa makazi na kulazimika kuhifadhiwa na majirani, huku wakazi kadhaa akiwemo Bi. Madawa Lukindo (80) wakijeruhiwa wakati wakijaribu kuokoa mali zao.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Bwana Hashim Mgandilwa, akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama, ametembelea maeneo hayo na kutoa maelekezo kwa ofisi ya Mkurugenzi kushughulikia hali hiyo.
Aidha, amewataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa kufuatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) zinazotabiri kuendelea kwa mvua zinazoweza kuleta madhara zaidi katika kipindi hiki.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)