Jamii ya watu wanaofuga nywele za mtindo wa rasta, maarufu kama Marasta, imekuwa ikitambulika kwa sababu mbalimbali iwe ni kwa misingi ya imani za kiroho, kufuata mitindo ya fasheni au kama njia ya kuonesha umaridadi na kujitofautisha na wengine.

Habari Wikiendi imemtembelea Erasto Kabuje mkazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe ambaye kwa zaidi ya miaka 20 sasa amekuwa akifuga nywele zake za mtindo wa rasta, zikiwa na urefu unaofikia miguuni na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wanaokutana naye.

Mwandishi wetu Emmanuel Kalemba anatueleza zaidi kuhusu safari yake ya kipekee ya kufuga Rasta.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @rajjmsangi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *