Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja wa unyang’anyi wa kutumia silaha uliofanyika Februari 4, 2026, saa 4:00 asubuhi, eneo la Kisimani, Unyamwanga, Kata ya Tunduma, Wilaya ya Momba.
Katika tukio hilo, mtuhumiwa na wenzake walimpiga risasi Yengo Mwapina na kumjeruhi kiunoni, kisha kumpora shilingi milioni 54, akiwa anatoka NBC Tunduma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Augustino Senga amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini mtandao wa wahalifu hao kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.
#AzamTVUpdates