Mfanyabiashara Lucy Oisso ameeleza kuwa utajiri wa mtu si wingi wa vitu alivonavyo, bali ni namna gani anafikiri kufikia malengo yake.
Oisso anasema ndoto za vijana wengi hazifanikiwi kwasababu hawapendi kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa na badala yake hukaa na kusema waliofanikiwa wametumia njia ambazo sio sahihi katika mafanikio yao japokuwa hawana uhakika wa kile wanachofikiri.
Mfanyabiashara huyo ameongeza kuwa hauwezi kujua mafanikio ya mtu bila kukaa na kujifunza kutoka kwake na kukuambia ni namna gani amefika hapo alipo sasa.
Oisso anasema kujifunza kwa watu waliofanikia ni jambo bora katika kutimiza malengo yako.
✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri | @allymufti_tz
#AzamTVUpdates