Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imekabidhi mashine za joto kwa ajili ya kutunzia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Radiant Warmer) na mashine za kutunzia watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa manjano (Phototherapy) katika Hospitali ya Rufaa ya Sokoine, Mkoani Lindi.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, ambaye amesema kuwa lengo la msaada huo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.

Imeandaliwa na Omary Mikoma
#AzamTVUpdates
Mhariri | @rajjmsangi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *