Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesisitiza kwamba Iran haitafanya mazungumzo kuhusu makombora yake, kwa sababu maudhui hiyo inahusu masuala ya ulinzi tu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mahojiano na Al Jazeera: “mazungumzo na Washington yalikuwa mwanzo mzuri, na hii ina maana kwamba yanaweza kuendelea kwa sura hii na kwa njia hii, na bila shaka, kungali kuna safari ndefu ya kujenga hali ya kuaminiana.”

Katika mahojiano hayo, Araghchi amesisitiza kwamba mazungumzo ya siku ya Ijumaa hayakuwa ya ana kwa ana, bali yalifanyika kupitia Oman, na yalihusu suala la nyuklia pekee.

Mbali na kubainisha kwamba kwa mtazamo wa Iran suala la marufuku urutubishaji urani haliwezi kujadiliwa na liko nje ya utaratibu wa mazungumzo, mkuu wa vyombo vya kidiplomasia vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: “rutubishaji urani ni haki ya Iran na lazima uendelee. Kiwango cha urutubishaji kinategemea mahitaji yetu, na urani iliyorutubishwa haitatolewa nje ya Iran. Sisi tuko tayari kupunguza kiwango cha urutubishaji. Wao hawakuweza hata kwa mashambulizi ya mabomu kuharibu uwezo wa Iran katika suala hili.”

Araghchi ameeleza kwamba, Iran iko tayari kufikia makubaliano ya uhakika kuhusu urutubishaji.

Kuhusu mpango wa makombora wa Iran, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu amesema: “hatuwezi kufanya mazungumzo kuhusu makombora sasa hivi wala katika siku zijazo kwa sababu hili ni suala la kiulinzi tu. Masuala ya eneo yanahusiana na eneo lenyewe na hayana uhusiano wowote na nchi zilizoko nje ya eneo hili. Mbali na hayo, hili ni suala la ndani linalowahusu watu wa Iran na hakuna upande wowote wa nje unaoweza kuingilia masuala yetu ya ndani. Tumelisema hili mara kadhaa.”

Araghchi amesisitiza kwa mara nyingine kwamba, kadhia ya nyuklia ya Iran inaweza kutatuliwa kupitia mazungumzo tu. 

Kuhusu uwezekano wa kutokea vita na majibu ya Iran kwa mashambulizi yanayowezekana kufanywa na Marekani, amesema: “uwezekano wa kutokea vita uko muda wote, na sisi tuko tayari kwa hilo na kwa ajili ya kuzuia vita visitokee. Hakuna uwezekano kwa sisi kushambulia ardhi ya Marekani ikiwa Marekani itatushambulia, lakini kama itaishambulia Iran, tutazishambulia kambi za Marekani katika eneo hil”…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *