Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imezitaka taasisi na mashirika ya serikali kuhakikisha yanatumia mfumo wa anuani za makazi ili kutoa huduma bora na haraka kwa wananchi.
Waziri wa Wizara hiyo, Anjela Kairuki, amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Wiki ya Anuani za Makazi, ambapo pamoja na mambo mengine, amesisitiza kuwa mfumo huo ni nguzo muhimu hasa wakati huu ambao nchi inaelekea kwenye uchumi wa kidijitali.
#AzamTVUpdates
Mhariri: @rajjmsangi