Katika kuhakikisha kunakuwepo suluhu ya kudumu ya utatuzi wa changamoto ya vituo vya kujazia gesi, Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kupitia ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, ili kukuza maendeleo ya taifa.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kituo cha kujaza gesi asilia kwa magari kilichopo Tegeta, akisisitiza umuhimu wa kutoa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi na ujenzi wa miundombinu.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *