Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia ameishutumu Eritrea jirani kwa uchokozi wa kijeshi na kuunga mkono makundi yenye silaha katika eneo la Ethiopia, kulingana na barua iliyoonekana na shirika la habari la Reuters na kuthibitishwa na wizara hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mahasimu hawa wawili wa muda mrefu, ambao walipigana vita kati ya mwaka 1998 na 2000, walisaini makubaliano ya amani mwaka wa 2018 na walikuwa washirika wakati wa vita vya miaka miwili vya Ethiopia dhidi ya mamlaka za mkoa huko Tigray, kaskazini mwa nchi.

Hata hivyo, Eritrea haikuwa imetia saini makubaliano ya mwaka 2022 yaliyomaliza mzozo wa Tigray, na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili umezorota sana tangu wakati huo.

Mapigano ya hivi karibuni kati ya vikosi vya Tigray na wanajeshi wa Ethiopia yamefufua hofu ya uhasama mpya.

Msemaji wa serikali ya Eritrea amesema kwamba mamlaka ilikuwa ikithibitisha kama barua hiyo imefika kwa Wizara ya Mambo ya Nje. Katika barua ya tarehe 7 Februari na iliyoandikwa kwa mwenzake wa Eritrea, Osman Saleh, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Gedion Timothewos alisema kwamba vikosi vya Eritrea vimekuwa vikichukua eneo la Ethiopia kwa muda mrefu kando ya mpaka wao wa pamoja na vilikuwa vikitoa msaada wa vifaa kwa makundi yenye silaha yanayoendesha harakati zao nchini Ethiopia.

“Kuingia kwa wanajeshi wa Eritrea ndani zaidi ya eneo la Ethiopia … si uchochezi tu, bali ni kitendo cha wazi cha uchokozi,” barua hiyo imesema, ikitaka vikosi vya Eritrea viondolewe mara moja na kukomeshwa kwa ushirikiano wote na makundi yenye silaha.

Gedion amedai kwamba matukio ya hivi karibuni yalionyesha “kuongezeka kwa vurugu,” akitaj luteka ya pamoja ya kijeshi kati ya vikosi vya Eritrea na makundi yenye silaha ya Ethiopia karibu na mpaka wa kaskazini magharibi.

Eritrea imejibu kwa hasira taarifa za umma zilizorudiwa na Waziri Mkuu Abiy Ahmed kwamba Ethiopia isiyo na bandari ina haki ya kufikia bahari – taarifa ambazo wengi nchini Eritrea, nchi iliyo karibu na Bahari Nyekundu, wanaona kama tishio lisilo wazi la hatua za kijeshi. Katika barua yake, Gedion amesema kwamba Ethiopia itaendelea kuwa wazi kwa mazungumzo ikiwa Eritrea itaheshimu uadilifu wake wa eneo. Ameongeza kuwa Addis Ababa ilikuwa tayari kushiriki katika mazungumzo ya nia njema kuhusu masuala yote yenye maslahi ya pamoja, ikiwa ni pamoja na masuala ya baharini na ufikiaji wa Bahari Nyekundu kupitia bandari ya Assab ya Eritrea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *