Magazeti ya Jumatatu, Februari 9, yanaripoti kwa upana maoni ya Rais William Ruto kuhusu mipango ya kufufua muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition.

papers
Magazetini: Fujo Baada ya Mwanafunzi wa KMTC Kuawa kwa Kupigwa Risasi.
Source: Facebook

Magazeti haya pia yanaripoti kuhusu mauaji ya Cheryl Adhiambo katika mtaa wa Huruma Estate, kaunti ya Nairobi.

1. Daily Nation

Mnamo Jumapili, Februari 8, maandamano yalizuka katika mtaa wa Huruma kaunti ya Nairobi kufuatia mauaji ya kutatanisha ya Cheryl Odhiambo, 21.

Mwanafunzi huyo wa Taasisi ya Mafunzo ya Matibabu(KMTC) alifariki akiwa ndani ya kibanda cha mamake cha samaki baada ya kupigwa risasi kwenye jicho lake na maafisa wa polisi waliokuwa wamejihami wakimfuata mhalifu.

Kisa hicho kilitumbukiza Huruma kwenye ghasia na machafuko yaliyoendelea usiku kucha hadi Jumapili adhuhuri.

“Nilikuwa nimeenda kumtembelea mtoto wangu shuleni nilipopigiwa simu na kufahamishwa binti yangu ameuawa. Nimeacha binti yangu mikononi mwa serikali. Sitaki kujua jinsi atakavyosafirishwa nyumbani kwa mazishi, jinsi suala lake litakavyoendelea, au iwapo atapata haki. Nimeachia serikali,” alisema Caroline Akinyi, mamake marehemu.

Polisi walithibitisha kuwa Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) imeanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo, huku maafisa wakiahidi ushirikiano kamili.

“Kufuatia tukio hilo, uvunjaji wa sheria na utaratibu umeshuhudiwa katika eneo hilo, na ripoti za magari mawili kuchomwa moto leo. Tunawahakikishia umma kwamba mchakato kamili wa uwekaji kumbukumbu na uwajibikaji kwa tukio hili unaendelea,” NPS ilisema.

2. The Standard

Rais William Ruto alimkashifu mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta, kuhusu mipango ya kufufua muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party kabla ya uchaguzi wa 2027.

Akizungumza Jumapili, Februari 8, rais alisema kwamba muungano wa upinzani hauleti tishio lolote kwa azma yake ya kuchaguliwa tena mwaka wa 2027.

Ruto alipuuzilia mbali juhudi mpya za Uhuru kupanga upya Azimio, akisema kuwa muungano huo hauna uzito wa kisiasa bila chama chake kikuu tanzu cha Orange Democratic Movement (ODM).

Kulingana na Ruto, upinzani unapaswa kujipanga kwa mchuano mkali katika uchaguzi mkuu ujao.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *