Mkuu wa vikosi vya Ulinzi vya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, na Kamanda wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, wamesisitiza kuwa, Iran haitafuti kuanzisha vita vya kikanda licha ya utayari wake kamili.

Maafisa hao wakuu wa jeshi nchini Iran wameonya kwamba ongezeko lolote la mapigano litavuruga utulivu wa eneo la Asia Magharibi kwa miaka mingi, huku wakisisitiza kwamba vikosi vya jeshi vinamfuatilia adui kwa karibu na vinaendelea kuwa tayari kujibu kwa dhati tishio lolote.

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi amesema mbele ya hadhara ya makamanda na wafanyakazi wa Jeshi la Anga na Vikosi vya Ulinzi wa Anga vya Jeshi la Iran na kueleza kwamba, “Licha ya utayari wetu, hatutaki kuanzisha vita vya kikanda. Ingawa wavamizi ndio wanaochochea vita vya kikanda, kuzuka kwake kwa vyovyote vile kutachelewesha maendeleo na ustawi wa eneo hili kwa miaka mingi na wachochezi wa vita, yaani Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel zinabeba dhima ya matokeo yake.”

Kwa upande mwingine, Kamanda wa Jeshi la Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, amesema kando ya mkutano wa makamanda, maafisa na wafanyakazi wa Jeshi la Anga la Iran na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi: “Tunamfuatilia adui kwa karibu, na tuko tayari kujibu kwa uthabiti uovu wowote.”

Hatami amesisitiza umuhimu wa uzoefu uliopatikana kutokana na operesheni ya vita vya siku 12 vya Kujihami Kutakatifu.

Akiwahutubu maadui, Meja Jenerali Hatami alisisitiza: “Tunatumai adui hatafanya kosa lingine, na ikiwa atafanya hivyo, basi Jeshi la Anga la Jeshi litachukua jukumu muhimu katika kulijibu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *