
Mahakama Kuu ya Tanzania imepanga kuanza tena kwa kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu kuanzia leo Jumatatu Februari 9 hadi Machi 6, 2026, mbele ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na Gaston Garubindi, mkurugenzi wa masuala ya sheria wa chama cha upinzani cha CHADEMA, kesi hiyo, iliyosajiliwa chini ya nambari 19605/2025, itasikilizwa na jopo la majaji watatu: D. Ndunguru, J. Karayemaha, na Kiwonde.
Garubindi alithibitisha kwamba Lissu, mwenyekiti wa kitaifa wa CHADEMA, alipokea taarifa rasmi kutoka kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu mnamo Januari 14, 2026.
Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025, wakati wa mkutano huko Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, na alikuwa amezuiliwa kwa siku 282 kufikia Januari 15, 2026.
Ikumbukwe kuwa, kesi hiyo kwa sasa ipo kwenye hatua ya mashahidi wa Jamhuri kuendelea kutoa ushahidi wao Mahakamani hapo, hata hivyo mara ya mwisho kutajwa Mahakamani, mshtakiwa (Tundu Lissu) ambaye anajitetea mwenyewe aliwasilisha mapingamizi kadhaa ambayo bila shaka leo upande wa Jamhuri wataanza kwa kuyajibu.