Miji mikuu mingi ya dunia imeendelea kushuhudia maandamano ya kulaani ukiukaji unaoendelea wa utawala wa Kizayuni wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Waandamanaji hao wanataka kukomeshwa vita vya maauajai ya kimbari na kuruhusiwa kuingizwa misaada ya kibinadamu. Barani Ulaya mji mkuu wa Ufaransa Paris ni miongoni mwa miji mikuuu ambayo imeendelea kushuhudia maaadamano ya kulaaani jinai za Israel na kutoa wito wa kuruhusiwa uingizwaji wa misaada ya kibinadamu huko Gaza. Maandamano ya Paris pia yalijumuisha kaulimbiu zinazowaunga mkono watu wa Sudan na Venezuela.

Katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, Jukwaa la Mshikamano na Palestina la Ankara liliandaa maandamano ya kulaani ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza. Waandamanaji walikusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Uturuki na kutoa nara na akaulimbiu dhidi ya Israel.

Aidha katika mji mkuu wa Tunisia Tunis, makumi ya watu wameshiriki katika tukio lililoandaliwa chini ya anuani: “Msimamo wa Hasira Dhidi ya Kuendelea Uchokozi”, lililoitishwa na wanaharakati kutoka vyama na mashirika kama vile Muungano wa Tunisia wa Kuunga Mkono Haki ya Wapalestina, Uratibu wa Hatua za Pamoja kwa ajili ya Palestina, na Mtandao wa Tunisia wa Kupinga Kuanzishwa Uhuusiano na Israel.

Huko Stockholm mji mkuu wa Sweden pia, mamia ya watu wanaounga mkono Palestina wameandamana kupinga uvunjaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza. Vyombo vya habari viliripoti kwamba mamia ya wafuasi wa Palestina walikusanyika katika Uwanja wa Odenplan katikati mwa Stockholm, kwa mwaliko wa mashirika ya kiraia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *