
Watu hamsini na watatu wamekufa maji au hawajulikani waliko baada ya boti iliyokuwa imewabeba wahamiaji 55 kuzama nje ya pwani ya Libya siku ya Ijumaa, Februari 6, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti. Watu hao 55 walikuwa ndani ya boti ambayo haikuwa na uwezo wa kubeba idadi hiyo ya watu, IOM imeeleza katika taarifa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Boti hiyo ilizama kaskazini mwa Zuwara, Libya, mnamo Februari 6. Katika taarifa, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti kwamba wanawake wawili wa Nigeria waliokolewa na mamlaka ya Libya. “Mmoja wa walionusurika alisema alipoteza mumewe, huku mwingine akisema alipoteza watoto wake wawili katika mkasa huo,” IOM imesema.
Kulingana na kurasa za manusura, boti hiyo, iliyokuwa imebeba raia kutoka Afrika, iliondoka Zawiya, karibu na Tripoli, jioni ya Februari 5, IOM imeongeza. Ilizama takriban saa sita baadaye baada ya kuvamiwa na maji.
Mkasa huo unafanya idadi ya wahamiaji walioripotiwa kufariki au kutoweka katika njia ya baji ya Mediterania ya Kati mwaka wa 2026 kufikia angalau 484, kulingana na IOM. Shirika hili la Umoja wa Mataifa linabainisha kuwa njia ya bahari ya Mediterania ya Kati ndiyo iliyo na vifo vingi zaidi duniani, ikiwa na vifo 1,340 vilivyorekodiwa mwaka jana.
IOM inasisitiza “hitaji la ushirikiano wa kimataifa ulioimarishwa na majibu yanayolenga ulinzi ili kupambana na mitandao ya biasahara ya wa magendo na biashara haramu ya binadamu, pamoja na kuanzishwa kwa njia salama na za kawaida za uhamiaji ili kupunguza hatari na kuokoa maisha ya watu.”