Mwanamuziki kutokea Puerto Rico, Bad Bunny ameweka historia kuwa mtumbuizaji wa kwanza wa onesho la kipindi cha mapumziko cha Super Bowl kutumbuiza kwa lugha ya Kihispania wakati wa onesho hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2026, katika Uwanja wa Levi’s uliyopo Santa Clara, huko Jijini California nchini Marekani.
Moja ya tukio lililowavutia mashabiki wengi wakati wa pafomansi hiyo ni kushuhudia ndoa iliyofungwa wakati wa shoo hiyo. Wanandoa hao wapya walimuomba Bad Bunny ahudhurie kwenye harusi yao. Bad Bunny akawaalika waende kufunga ndoa yao wakati wa shoo yake ya Super Bowl Halftime.
Mwanamuziki Bad Bunny raia wa Puerto Rico akitumbuiza katika onesho la kipindi cha mapumziko cha Super Bowl usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2026, katika Uwanja wa Levi’s uliyopo Santa Clara, California nchini Marekani.
Tukio hilo lilifanyika wakati ambapo Lady Gaga alijiunga na Bad Bunny kutumbuiza wimbo wa wao wa “Baile Inolvidable,” wanandoa hao waliweka nadhiri pamoja huku Bad Bunny akiwa shahidi na kutia sahihi cheti chao cha ndoa.
Aidha, Bad Bunny kwenye Super Bowl Halftime Show alimkabidhi mtoto Lincoln Fox tuzo yake ya Grammy, akiashiria kisa cha mtoto aitwaye ‘Liam Conejo Ramos’ aliyekamatwa na maafisa wa uhamiaji (ICE) nchini Marekani mapema mwezi Januari mwaka2026.
Mwanamuziki Bad Bunny raia wa Puerto Rico akitumbuiza katika onesho la kipindi cha mapumziko cha Super Bowl usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2026, katika Uwanja wa Levi’s uliyopo Santa Clara, California nchini Marekani.
Wadau wengi wakitafsiri kuwa hiyo yote nikupinga kinachoendelea kwa wakazi wa Marekani na maafisa wa Uhamiaji (ICE).
Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump amelikosoa onesho hilo la Super Bowl LX half time show katika chapisho lake la mtandao, akiliita baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya onesho hilo maarufu Marekani.
Mwanamuziki Bad Bunny raia wa Puerto Rico akitumbuiza katika onesho la kipindi cha mapumziko cha Super Bowl usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2026, katika Uwanja wa Levi’s uliyopo Santa Clara, California nchini Marekani.
Trump amepinga mtindo wa uwasilishaji wa onesho hilo msimu huu, akisema kuwa haukufikia matarajio ya kawaida ya maonesho mengine ya Super Bowl yaliyowahi kufanyika.
Maoni hayo yameibua hisia na mjadala mtandaoni wengi wakitafsiri yote haya yanatokea kutokana na nyota huyo wa Purto Rico kuonesha kumpinga wazi wazi rais huyo wa Marekani kutokana na jinsi anavyotekeleza mpango wake wa kuwafukuza wahamiaji katika nchi ya Marekani.
Sambamba na hayo, mwanamuziki nyota kutoka nchini Marekani Chris Brown, kupitia chapisho aliloweka katika ukurasa wake wa Instagram limetafsiriwa kama dongo kwenda kwa waandaaji wa tamasha hilo, NFL na Apple Music.
Maoni yake baada ya muda mchache wa performance ya ‘Bad Bunny’ kwenye Super Bowl LX Halftime Show, Breezy aliandika “Nadhani ni sahihi nikisema wananihitaji mimi”
Mwanamuziki Bad Bunny raia wa Puerto Rico akitumbuiza katika onesho la kipindi cha mapumziko cha Super Bowl usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2026, katika Uwanja wa Levi’s uliyopo Santa Clara, California nchini Marekani.
Msanii aliyepewa jukumu la kutumbuiza wakati wa mapumziko wa Super Bowl 2026, Benito Antonio Martínez Ocasio, Bad Bunny ni mmoja wa wasanii wenye streams nyingi zaidi duniani na anazingatiwa kama mwanamuziki bora wa Kilatini wa karne ya 21.
Sifa yake kwenye majukwaa ya kimuziki ni kubwa, kwani ni mshindi wa tuzo kubwa za Grammy mara 6, na kwa mwaka 2026 alinyakua tuzo hizo tatu ambazo ni Album of the year “DeBÍ TiRAR MáS FOToS”, Best Global Music Performance: “EoO”, Best Música Urbana Album: “DeBÍ TiRAR MáS FOToS” ushindi huo ulimfanya kuwa msanii wa pili baada ya Kendrick Lamar aliyeondoka na tuzo tano usiku huo.
Bad Bunny anakuwa sio msanii wa kwanza kupafomu katika jukwaa la Super Bowl Half Time Show utakumbuka 2025 alipafomu rapa Kendrick Lamar, 2024 alifanya Usher Raymond, 2023 Rihanna, 2022 walipafomu Dr.Dre. Snoop Dogg, Eminem, Mary J, 50 Cent, pamoja na Kendrick Lamar.