Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema uteuzi wa watendaji wa nafasi mbalimbali alioufanya hivi karibuni, umelenga kuongeza kasi ya utendaji, kuimarisha uwajibikaji, kulinganisha majukumu na vipaumbele vya Taifa na kuendana na kasi ya matarajio ya wananchi.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Februari 9, 2026 alipozungumza katika hafla ya kuwaapisha wateule wake, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Lengo ni kuendana na kasi ya matarajio ya wananchi. Mmeaminiwa kwa uwezo, uzoefu na uadilifu. Niwatake mkaishi na kiapo mlichoapa hapa leo, lakini pia kuna kiapo cha maadili mmesaidi nakala mbili,” amesema.
#StarTvUpdate