Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewataka watendaji wote aliowateuwa na kuwaapisha, kuhakikisha wanaifanya Tanzania iendelee na wasimamie utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.
Dkt Samia ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu Februari 9, 2026 alipozungumza katika hafla ya kuwaapisha wateule wake, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Sisi ndio wa kuweka msingi kama tulivyota msingi wengine wameweka sisi tukajenga juu, na sisi ndio wa kuweka msingi wa utekelezaji wa dira tunayokwenda kuitekeleza, kwa hiyo niombe kila mtu akatekeleze wajibu wake,” amesema.
#StarTvUpdate