Rais Samia Suluhu Hassan amesema Soko jipya la Kariakoo limejengwa kwa kodi za wananchi na ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ili kuweka mazingira mazuri ya kufanyia biashara.
Akizungumza katika uzinduzi wa soko la Kariakoo jana 08.02.2026 jijini Dar es Salaam Rais Samia amewataka wafanyabiashara ndani ya soko hilo kuendelea kulipa kodi stahiki kwa wakati ili miradi mingine ya Serikali iendelee kujengwa yakiwemo masoko.
Amezitaka Mamlaka zinazohusika na ukusanyaji wa kodi ikiwemo Halmashauri ya Ilala na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya kazi kwa uaminifu na ushirikiano ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kuepuka ukwepaji kodi.
Aidha Rais Samia amehimiza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha kila mmoja analipa kiwango anachotakiwa kulipa.
#StarTvUpdate