Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilikuwa na ndege zisizo na rubani mpya 85 mwanzoni mwa mwez Januari, kulingana na Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu katika Chuo Kikuu cha Yale, ambayo imefikia makadirio haya kulingana na uchambuzi wa picha za setilaiti. Taasisi hiyo pia inasema kwamba nyingi kati ya ndege hizo zilitolewa na Falme za Kiarabu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchini Sudan, Vikosi vya Msaada wa Haraka vya Jenerali Hemedti (RSF) vimeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wao wa mashambulizi ya anga katika miezi ya hivi karibuni. Baada ya kuchanganua picha za setilaiti, Maabara ya Utafiti wa Kibinadamu katika Chuo Kikuu cha Yale inakadiria kwamba wanamgambo hao wa RSF walikuwa na ndege zisizo na rubani mpya 85 mwanzoni mwa mwezi wa Januari. Kulingana na watafiti, 40 kati ya ndege hizi zilikuwa katika eneo ilililo karibu na Uwanja wa Ndege wa Nyala, makao yao makuu huko Darfur Kusini. Nyingine hamsini na moja zilikuwa katika eneo lililoko takriban kilomita mbili kutoka kambi ya zamani ya Ujumbe wa Pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur (UNAMID). Mwishoni mwa mwezi Januari, zaidi ya nusu ya ndege hizi hazikuwepo tena sehemu hizo.

“Hatujui gharama ya kila ndege isiyo narubani, lakini drone pamoja na vifaa vyake ikiwa ni pamoja na risasi na makombora inauzwa mamilioni ya dola,” anaelezea Olivia Mooney, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Yale, ambaye anabainisha kwamba RSF ilipokea msaada kutoka nje ili kuzipata. Ananyooshea kidole kwa “Falme za Kiarabu, kuna uwezekano mkubwa. Ni muhimu kuelewa kwamba hizi ni drone za teknolojia ya juu sana zinazoweza kurushwa mamia ya kilomita,” anaongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *