Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, imeahirishwa mpaka Februari 11 , 2026 ambapo Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi baada kusikiliza hoja za kisheria za pande zote mbili kuhusiana na uhalali wa mashahidi fiche wa Jamhuri.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kulingana na Gaston Garubindi, mkurugenzi wa masuala ya sheria wa chama cha upinzani cha CHADEMA, kesi hiyo, iliyosajiliwa chini ya nambari 19605/2025, itasikilizwa na jopo la majaji watatu: D. Ndunguru, J. Karayemaha, na Kiwonde.

Garubindi alithibitisha kwamba Lissu, mwenyekiti wa kitaifa wa CHADEMA, alipokea taarifa rasmi kutoka kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu mnamo Januari 14, 2026.

Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025, wakati wa mkutano huko Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, na alikuwa amezuiliwa kwa siku 282 kufikia Januari 15, 2026.

Ikumbukwe kuwa, kesi hiyo kwa sasa ipo kwenye hatua ya mashahidi wa Jamhuri kuendelea kutoa ushahidi wao Mahakamani hapo, hata hivyo mara ya mwisho kutajwa Mahakamani, mshtakiwa (Tundu Lissu) ambaye anajitetea mwenyewe aliwasilisha mapingamizi kadhaa ambayo bila shaka upande wa Jamhuri utaanza kwa kuyajibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *