Zanzibar. Mwanamuziki Benard Paul, Ben Pol anasema haijalishi umetokea wapi malengo uliyonayo yanaweza kukuweka sehemu ambayo hukutarajia.
Ben Pol amesema hayo baada ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye jukwaa la kimataifa la Sauti za Busara lililofanyika Zanzibar kuanzia Februari 5-8,2026.
“Mimi nimetokea kwenye familia ambayo haina msanii, msomi wala koneksheni natamani niwaoneshe vijana wenzangu nilipotoka na waone sasahivi,”amesema.
Ben Pol akitumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara
Akizungumzia uwezo wa kuwakosha mashabiki wa mataifa mbalimbali kwa kutumia lugha ya kiswahili kwenye nyimbo zake amesema muziki pekeyake tayari ni lugha.
“Unajua muziki ni lugha ambayo inaeleweka na mtu yeyote. Wakati tunatengeneza playlist studio tulisema tunataka kutengeneza ambayo kila mtu anaweza kusikia na kucheza kwamba hamna mtu atabaki nyuma.
Ben Pol akiwa kwenye chumba cha wasanii, katika tamasha la Sauti za Busara
“Maandalizi hayakuwa na ugumu wowote. Mara nyingi sisi tulikuwa tunafanya mazoezi ya muda tu kwa sababu tulipewa dakika 50. Lakini sio mazoezi ya ufansi kwa sababu wote wapo vizuri,”amesema
Hatahivyo msanii huyu hakuacha kutoa shukrani zake kwa kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye jukwaa hilo.
“Kwanza nashukuru jukwaa la Sauti za Busara kwa kutupa nafasi. Mimi nina miaka 16 kwenye muziki, lakini ndiyo kwanza kama naanza nikikaa na bebdi nawaza tufanye kitu gani ili tutoke. Hii ni kazi yetu kwahiyo tutakutana kwenye Grammy na sehemu nyingine,”amesema
Utakumbuka Ben alitumbuiza siku ya pili ya tamasha hilo.Kati ya nyimbo alizoimba jukwaani ni Sofia, Maneno na nyinginezo.