PWANI: Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuzindua miradi mikubwa ya kuendeleza utalii Kusini kesho.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Hassan Abbasi leo Februari 9, 2026 amekagua maandalizi ya uzinduzi wa miradi ya kuendeleza utalii kusini.

Miradi hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa hapo kesho imejengwa katika hifadhi za Taifa za Julius Nyerere, Mikumi, Ruaha pamoja na Msitu wa Asili Kilombero na imegharimu zaidi ya Sh bilioni 100.
Uzinduzi wa Miradi hiyo mikubwa iliyojengwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa dhumuni la kukuza na kuendeleza utalii kusini mwa Tanzania utafanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere.