Eritrea imekanusha madai ya Ethiopia kuwa wanajeshi wake wapo katika nchi hiyo jirani, madai wanayosema ni ya uongo na yaliyotengezwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Eritrea inakuja, wakati huu Ethiopia ikiishtumu kwa kuwatuma wanajeshi wake, katika nchi hiyo, kuwaunga mkono makundi yenye silaha.

Siku ya Jumamosi iliyopita, Ethiopia iliambia Eritrea, kuwaondoa wanajeshi wake katika ardhi yake, madai ambayo Waziri wa Habari wa Eritrea Yemane Gebremeskel amesema ni uongo mwingine unaotengezwa kulipata tope taifa lake.

Aidha, amesema Eritrea haina haja ya kurushiana maneno na Ethiopia kuhusu madai yake kuwa inawaunga mkono makundi yenye silaha katika jimbo la Amhara.

Hata hivyo, Ethiopia imesimamia kauli yake na kuishtulmu Eritrea kwa uvamizi wa nchi yake.

Majibizano haya yamekuja licha ya nchi hizo jirani kushirikiana kati yam waka 2020 hadi 2022 kulikabili kundi la Tigray, lakini mataifa hayo yakatofautiana kuhusu mkataba wa amani uliomaliza vita hivyo, vilivyosabisha vifo vya watu  600,000. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *