
Milio ya risasi imesikika asubuhi ya leo katika Gereza Kuu la Kaloum, kituo cha utawala cha Conakry. Kulingana na mashahidi waliowasiliana na RFI, risasi hizo zilianza kuskika saa 9:00 usiku (saa za Guinea) na zilidumu kwa takriban nusu saa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kisha barbara ya kufika katikati ya jiji ilifungwa na jeshi kabla ya kufunguliwa tena muda mfupi kabla ya saa 11:00 alfajiri. Polisi na wanajeshi walifunga mitaa inayoelekea gerezani asubuhi, na magari ya wagonjwa pia yalikuwa yameegeswa katika eneo la tukio.
Wafungwa wengi mashuhuri wanashikiliwa katika gereza hili, wakiwemo wanajeshi wa zamani waliohusika katika mauaji ya Septemba 28, 2009 na mawaziri wa zamani wa Alpha Conde.
Mamlaka bado haijatoa tangazo lolote kuhusu tukio hili.
Ikumbukwe kwamba gereza hili lililengwa na shambulio mnamo mwaka 2023. Kundi la watu waliojihami kwa silaha nzito lilimtorisha Kapteni Moussa Dadis Camara. Kitendo chao kilisababisha vifo kadhaa.
Operesheni ya kumuhamisha Kamanda Toumba Diakité ilipangwa kufanyika siku ya Jumanne, Februari 10. Hata hivyo, operesheni hiyo ilifanyika. Alipelekwa mahali pasipojulikana.