
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonyesha wasiwasi mkubwa na kulaani uamuzi wa hivi karibuni wa Israel wa kuidhinisha hatua zinazorahisisha upanuzi wa makaazi ya walowezi wa Kizayuni na kupanua udhibiti wa kiutawala na utekelezaji wa sheria wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amebaini wasiwasi mkubwa na kulaani uamuzi wa hivi karibuni wa Israel wa kuidhinisha hatua zinazorahisisha upanuzaji wa makaazi ya walowezi wa Kizayuni na kupanua udhibiti wa kiutawala na utekelezaji wa sheria wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan unaokaliwa kwa mabavu.
Guterres ameoa kauli hiyo siku ya Jumatatu, kufuatia lawama kama hizo kutoka kwa nchi za kanda ambazo zimelaani hatua ya Israel na kuitaja kuwa ni mwendo kuelekea kunyakua eneo hilo.
Hatua hizo, zilizoidhinishwa na baraza la mawaziri la usalama la Israel tarehe 8 Februari 2026, zinajumuisha kulegeza vikwazo kwa walowezi Wayahudi kununua ardhi katika eneo hilo, kuondoa usiri katika kumbukumbu za usajili wa ardhi, na kupanua mamlaka ya utekelezaji ya Israel katika Maeneo A na B, ambayo kwa mujibu wa Mikataba ya Oslo yako chini ya mamlaka ya Mamlaka ya Palestina.
Kupitia msemaji wake, Stéphane Dujarric, Guterres amesisitiza tena kwamba makaazi yote ya Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, ikiwemo al‑Quds Mashariki, pamoja na mifumo na miundombinu yake, hayana uhalali wa kisheria na ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na maazimio husika ya Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Ulaya pia umelaani uamuzi huo, ukieleza kuwa ni hatua nyingine katika mwelekeo usio sahihi inayozidi kutatiza juhudi za amani.
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali vitendo vya Israel, ikivielezea kuwa ni sehemu ya sera yake endelevu ya kikoloni, na kusema sera hizo za Israel ni uhalifu wa kivita pamoja na ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Nchi kadhaa za Waislamu ,ikiwemo Saudi Arabia, Jordan, Misri, Indonesia, Falme za Kiarabu, Uturuki, Qatar na Pakistan zimetoa tamko la pamoja zikilaani hatua hizo kwa maneno makali zaidi.
Nchi hizo zimesema uamuzi huo ni jaribio haramu la kulazimisha mamlaka ya Israel juu ya ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo, hatua inayodhoofisha utulivu wa kikanda na maono ya mataifa mawili.
Makundi ya mapambano ya ukombozi ya Palestina kama vile Hamas na Jihad Islami yamesisitiza ulazima wa kukabiliana na mipango ya Wazayuni wenye misimamo mikali katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.