
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov amesema, mtindo mchafu wa maisha wa mfadhili na mhalifu wa vitendo vya ngono wa Marekani Jeffrey Epstein pamoja na tapo lake ni ushuhuda wa kuporomoka kimaadili shakhsia muhimu na maarufu wa Magharibi.
Lavrov ameyasema hayo katika mahojiano na chaneli ya televisheni ya NTV na kubainisha: “mafaili hayo yamefichua sura ya Magharibi na genge linalodhibiti serikali, au tuseme zaidi muungano wa kina unaoitawala Magharibi yote na unaotaka kuutawala ulimwengu mzima”.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameongezea kwa kusema: “mtu yeyote wa kawaida anajua kwamba hiki ni kitu kisichoweza kufahamika hata kidogo na ni ushetani halisi”.
Epstein alifariki mwaka 2019 akiwa kwenye chumba cha gereza la New York nchini Marekani katika kile kilichoelezwa kuwa ni tukio la kujiua. Mpenzi wake wa zamani na mshirika wake wa karibu katika tapo la uhalifu wa kingono alilokuwa akiendesha Ghislaine Maxwell, yeye alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela mwaka 2022 kwa kupatikana na hatia ya kufanya biashara haramu ya kusafirisha na kuwadhalilisha wasichana wadogo kiumri kwa kushirikiana na Epstein.
Katika maisha yake yote ya kujihusisha na vitendo vichafu vya kingono, Epstein alishirikiana na wanasiasa mashuhuri wa Magharibi, wanadiplomasia, wafanyabiashara, na familia za kifalme, ambao wengi wao walitembelea kisiwa chake cha binafsi cha Karibiani.
Nyaraka zilizotolewa hivi karibuni zinaonyesha kuwa, Epstein na washirika wake walishiriki hata katika mila za kishirikina zinazohusisha utoaji kafara ya wanadamu. Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk alitangaza wiki iliyopita kwamba serikali yake itachunguza kama watoto wa nchi hiyo walifanyiwa vitendo vya udhalilishaji ikiwa ni sehemu ya kile kinachoitwa “tapo la kishetani” la Epstein…/