
Kamisheni hii ni chombo cha ushauri kinachohusika na nguzo ya maendeleo ya kijamii kwa maendeleo ya kimataifa.
Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa amezungumza na mmoja wa waliohudhuria mkutano wa mwaka huu akiwakilisha Tanzania; Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na anaanza kwa kueleza zaidi kuhusu mkutano huu.