
Nchini Senegal, kesi inayohusisha ushoga na shutuma za kusambaza VVU kimakusudi imeibua hisia kali kwenye vyombo vya habari na kisheria. Wanaume kumi na wawili—wakiwemo watu wawili mashuhuri—wamekamatwa na polisi kwa makosa kadhaa, ikiwa ni pamoja na “vitendo dhidi ya maumbile,” kosa la jinai nchini humo. Washukiwa wamefikishwa mbele ya jaji.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Dakar, Juliette Dubois
Polisi wa Senegal walitangaza kukamatwa kwa wanaume kumi na wawili, walioshtakiwa kwa “njama ya jinai,” “vitendo dhidi ya maumbile,” “kuhatarisha maisha ya wengine,” na “kusambaza VVU kimakusudi.” Miongoni mwao ni watu wawili mashuhuri wa vyombo vya habari: mtangazaji wa redio na televisheni Pape Cheikh Diallo, na mwanamuziki Djibril Dramé.
Kulingana na mamlaka, baadhi ya washukiwa wana VVU – jambo lililosababisha wachunguzi kuwashtaki kwa “kusambaza VVU kimakusudi,” kosa chini ya sheria ya Senegal iliyoanza mwaka 2010 – na wanakabiliwa na faini na vifungo vya hadi miaka 10 jela. Mahusiano ya ngono ya jinsia moja yamepigwa marufuku nchini Senegal chini ya kanuni ya adhabu na yanaadhibiwa kwa kifungo cha mwaka mmoja hadi mitano jela.
Suala hili ni mada ya mjadala unaojirudia nchini humo, ambapo ushoga unanyanyapaliwa sana. Kabla ya kuingia madarakani, Waziri Mkuu wa sasa, Ousmane Sonko, alitangaza nia yake ya kuimarisha utekelezaji wa sheria kwa kupendekeza adhabu kali zaidi. Watu kumi na wawili waliohusika walifikishwa mbele ya jaji siku ya Jumatatu, Februari 9. Uchunguzi wa mahakama umefunguliwa.
Kuwatisha na kuwanyanyapaa watu wa jamii ya LGBT
Siku ya Jumatatu, Februari 9, shirika linapinga ubaguzi kwa wapenzi wa jinsi moja, Stop homophobie, ambalo linafanya kazi nchini Senegal, lilielezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu kukamatwa kwa watu hao.
“Mashtaka haya mara nyingi hayahusiani kabisa na ukweli uliothibitishwa bali hutumika kuwatisha na kuwanyanyapaa watu wa jamii ya LGBT. Kwa bahati mbaya, yanaimarisha wazo kwamba ushoga ni hatari na, kijamii, huhalalisha ukandamizaji. Hii ndiyo sababu mamlaka mara nyingi hushtaki kwa maambukizi ya VVU kwa makusudi (…) Wasiwasi wetu ni kuona haki za msingi za watu wa LGBT zikikiukwa na maisha yakihatarishwa kwa sababu ya jinsi walivyo, amesema Terrence Katchadourian” , Katibu Mkuu wa shirika linalopinga ubaguzi kwa wapenzi wa jinsi moja.