India. Baada siku 13 kupita tangu mwanamuziki wa India, Arijit Singh, kutangaza kuacha muziki. Hatimaye ameonekana akitumbuzia kwenye moja ya show jijini Kolkata.
 
Wikiendi iliyopita Arijit alipanda jukwaani kwa mara ya kwanza baada ya kutangaza kuacha muziki. Ambapo alitumbuiza katika ukumbi wa ‘Netaji Indoor Stadium’ akishirikiana na mastaa Anoushka Shankar pamoja na Bickram Ghosh.

Usiku huo Arijit alifanikiwa kuimba nyimbo mbalimbali ikiwemo Maya Bhora Raati. Wimbo wa asili wa Kibengali uliowahi kuimbwa na Lakshmi Shankar na kutungwa na Pandit Ravi Shankar. 

Aidha baada ya kutumbuiza msanii huyo alichukua maiki na kuzungumza kidogo akisema ‘Nina wasiwasi sana sijui ni kwanini lakini asanteni kwa kunikaribisha kwa mara nyingine,”

Hata hivyo tukio hilo limewafurahisha mashabiki wengi katika mitandao ya kijamii, wakimpongeza kwa kufanya uamuzi mzuri wa kurudi katika muziki. Huku baadhi wakimponda wakimuita mtu asiye na msimamo.

Utakumbuka Januari 27,2026, Arijit alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba hatapokea tena kazi mpya za uimbaji wa playback. “Habari, heri ya Mwaka Mpya kwenu nyote. Napenda kuwashukuru kwa upendo mkubwa mlionipa kwa miaka yote kama wasikilizaji. Nina furaha kutangaza kwamba kuanzia sasa sitachukua tena kazi mpya kama mwimbaji wa playback. Nimeamua kuhitimisha safari hii. Ilikuwa safari ya kupendeza sana,”

Aidha wakati wa mahojiano yake baada ya tangazo hilo alitoa sababu zilizomfanya achukue uamuzi wa kujiondoa kwenye uimbaji wa playback. Ambapo alieleza zipo sababu nyingi mojawapo ni kupoteza ushawishi.

Arijit alianza rasmi muziki mwaka 2005 akiwa mshiriki wa shindano la Fame Gurukul. Alifanya debut yake katika filamu za Kihindi kupitia wimbo Phir Mohabbat kutoka Murder 2 mwaka 2011, kisha akajipatia umaarufu mkubwa India kupitia wimbo Tum Hi Ho kutoka Aashiqui 2 ya mwaka 2013.

Kwa miaka iliyofuata, Arijit ametoa nyimbo nyingi ambazo zilipendwa zaidi na mashabiki, zikiwemo Channa Mereya, Agar Tum Saath Ho, Raabta, Kesariya, Ae Dil Hai Mushkil, Tera Yaar Hoon Main na Tujhe Kitna Chahne Lage. 

Kazi yake ya hivi karibuni ya playback ni wimbo Hum To Tere Hi Liye The kutoka kwenye filamu ijayo ya Vishal Bhardwaj, O Romeo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *