
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi ametangaza siku ya Jumanne, Februari 10, kwamba atasafiri kwenda Moscow mwezi Machi kujadili suala la Wakenya kadhaa walioajiriwa kwa nguvu katika jeshi la Urusi kwa lengo la kupigana nchini Ukraine. Huku akiona njia hiyo “haikubaliki na ni ya siri,” anakusudia kuitembelea Urusi katika hali ya kuimarisha uhusiano na moyo wa kujenga.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaëlle Laleix
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi alitangaza binafsi siku ya Jumanne, Februari 10, kwamba atasafiri kwenda Urusi mwezi Machi kujadili suala la Wakenya walioajiriwa kwa nguvu katika jeshi la Urusi kupigana nchini Ukraine. Kulingana na makadirio ya Nairobi, kuna takriban watu 200 kama hao, ambao walisafiri kwebda nchini Urusi chini ya ahadi ya ajira ambayo iligeuka kuwa mikataba na vikosi vya jeshi la Urusi.
Akielezea njia hii kama “haikubaliki na ya siri,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya hata hivyo anakusudia kusafiri kwenda Moscow kwa moyo wa kujenga. “Kwa maoni yangu, haya yote yanawakilisha tukio baya katika uhusiano mzuri na chanya ambao nchi zetu mbili zimedumisha […] tangu uhuru,” aliiambia BBC. Majadiliano yatalenga kupambana na vitendo vya kuajiri watu kinyume cha sheria, pamoja na masuala ya visa na mikataba ya ajira ya pande mbili ambayo haijumuishi kuajiri watu kwa ngu katika jeshi.
Nchini Kenya, mamlaka zinadai kwamba zimechukua udhibiti thabiti wa suala hili na kuelezea kwamba tayari zimewarudisha raia wao 27 kutoka Urusi, ambao sasa wanapokea usaidizi wa kisaikolojia. Zaidi ya mashirika 600 ya kuajiri watu yenye vitendo vya kutiliwa shaka yamefungwa, dai linalopingwa na kiongozi wa jamii huko Gatundu, Kaunti ya Kiambu, kaskazini mwa Nairobi. Wakati akijaribu kuwarudisha vijana wapatao kumi waliokwama nchini Urusi, haswa huko Novgorod, Micheal Kariuki ameiambia RFI kwamba “wote waliajiriwa na shirika moja” na kwamba “mitandao ya kuajiri bado inafanya kazi.”