Avión en Nueva Zelanda

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Atahualpa Amerise
    • Nafasi, BBC News Mundo
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

New Zealand imekumbwa na wimbi jipya la wananachi kukimbia. Zaidi ya raia 70,000 waliiondoka nchi yao katika kipindi cha mwaka mmoja pekee, takriban 1.4% ya idadi ya watu wake milioni 5.1. Watu wanaondoka ni wengi na wimbi ni kubwa kuliko ilivyokuwa kwa miongo kadhaa na kumeanza kuashiria mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi.

Mwelekeo huu haujakuwa wa muda mfupi kama zamani. Hadi hivi karibuni, wananachi wengi kuondoka kulihusisha vijana waliomaliza shule au chuo kikuu, wakienda Australia kwa miaka michache na kurudi. Sasa, wengi wa wanaondoka ni wafanyakazi wenye uzoefu, wakiwemo watu wenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 30, wakienda bila kuwa na mpango wa kurudi. Kati ya wanaondoka kwa mwaka ni wastani wa robo tu huerejea nchini humo.

Raia hawa wanahama kwa sababu ya ushindani mkubwa kutoka Australia, soko duni la ajira, na hali ya uchumi unaosuasua. Australia inaajiri raia wengi wa New Zealand, inatoa mishahara ya juu na fursa za maendeleo ambazo hazionekani ndani ya New Zealand. Sekta kama afya, polisi, ujenzi, na madini imekuwa kivutio kikubwa, huku idadi ya wauguzi na walinzi wakihama kusaka fursa bora za kazi na malipo mazuri.

Aeropuerto en Nueva Zelanda

Chanzo cha picha, Getty Images

Uchumi na soko la ajira duni

Uchumi wa New Zealand umekuwa na ukuaji wa wastani wa takriban 1% mwaka 2025, huku mishahara ikiongezeka taratibu.

Kiwango cha ajira kisichozidi 5.3% ni cha juu zaidi katika takriban muongo mmoja, huku idadi kubwa ya wafanyakazi wa sekta ya umma wakipoteza nafasi zao.

Watu wengi wanahisi uwezo wao wa kununua kupungua, hali inayosababisha familia nyingi kutafuta njia mbadala za kipato na fursa za maisha bora.

Pia, kwa mujibu wa wataalamu, kupungua kwa ajira katika miji mikubwa na sekta za msingi kunachochea vijana na wafanyakazi wenye ujuzi kuhamia nje ya nchi.

Kwa mara ya kwanza, uhamaji wa sasa unahusisha watu ambao tayari wameshaingizwa katika soko la ajira, si tu wanaomaliza vyuo au elimu fulani.

Watu hawa wanataka fursa za maendeleo za muda mrefu, ambazo mara nyingi zinapatikana zaidi katika nchi jirani ya Australia.

Mujer en Auckland

Chanzo cha picha, Getty Images

Hali ya uchumi unaosuasua imezidishwa na kupungua kwa uwezo wa watu kununua bidhaa, ambapo mishahara ya wastani ni ya kawaida kulinganisha na gharama za nyumba, chakula, na huduma nyingine za msingi.

Shinikizo hili limeifanya Australia kuwa kivutio kikubwa, kwani mishahara, malipo ya ziada, na fursa za ajira zinaonekana kuwa na faida kubwa zaidi.

Hii inasababisha mwelekeo mpya wa uhamaji, ambapo si tu vijana wanahama kwa muda mfupi, bali pia wafanyakazi wenye uzoefu na familia zao wanapanga kuhamia huko.

Wataalamu wanasema hili ni jambo la kipekee na halijawahi kushuhudiwa kwa kiwango hiki katika historia ya New Zealand.

Hombre caminando en Wellington

Chanzo cha picha, Getty Images

Australia kimbilio muhimu

Karibu 60% ya raia wa New Zealand wanaoondoka huenda Australia, nchi jirani yenye ajira nyingi na mishahara ya juu. Sekta za afya, polisi, ujenzi, na madini zinawavutia zaidi, huku mashirika ya Australia yakitoa usaidizi wa makazi na malipo ya ziada. Mfano ni wauguzi zaidi ya 10,000 waliokuwa wakiishi New Zealand walienda Australia mwaka mmoja uliopita kwa ajira bora.

Soko la kazi la Australia ni lenye nguvu na lina fursa nyingi kwa kila kipengele cha taaluma. Wafanyakazi wanapata bonasi za kufanya kazi mwishoni wa wiki, malipo ya ziada, na hali bora za kazi ambazo hazina uhakika ndani ya New Zealand.

Pia, jamii za wahamiaji zimeunda mtandao mzuri wa kijamii, ikiwapa raia wa New Zealand hisia ya urahisi wa kuhamia na kujiunga na familia au marafiki.

Manifestación de trabajadores

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa raia wa New Zealand waliozaliwa nje ya nchi, kuhamia Australia kunawawezesha kuungana na familia na jamii zao. Na wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kuzua maswali ya mustakabali wa taifa hilo..

Mchango wa ‘diaspora’ huu ni mkubwa kutikisa nchi, kwani raia zaidi ya 800,000 wa New Zealand na watoto wao wanaoishi nje ya nchi ni moja ya idadi kubwa zaidi ikilinganishwa na idadi ya wananchi. Hali hii inaonyesha jinsi uhamaji unaoendelea unavyoathiri taifa kwa muda mrefu.

Policías de NZ

Chanzo cha picha, Getty Images

3. Athari kwa taifa na suluhisho zinazopendekezwa

Uhamaji unaoendelea unaleta upotevu wa vipaji na ujuzi, kupungua kwa uzalishaji, na kushuka kwa ukuaji wa uchumi.

Sekta muhimu za taifa zinapoteza wafanyakazi wenye uzoefu, hali inayosababisha changamoto za muda mrefu kwa ukuaji wa uchumi na ushindani wa kimataifa.

Serikali ya New Zealand imeahidi kurekebisha kodi na kanuni ili kuvutia na kuhifadhi talanta, huku pia ikilenga kuvutia wafanyakazi wenye ujuzi kutoka nje. Wengi wao kutoka nchi zikiwemo za Afrika.

Hata hivyo, wataalamu wanasema hatua hizi hazitoshi, kwani uchumi wa New Zealand unaendelea kusuasua ikilinganishwa na fursa zinazotolewa na Australia.

Wellington

Chanzo cha picha, Getty Images

Aidha, serikali haijaweka mkakati madhubuti wa kuungana na wananachi wanaoishi ama kukimbilia nje ‘diaspora’ au kutumia uzoefu na mitandao ya raia wake walioko nje ya nchi.

Hii ni hasara, kwani ‘diaspora’ inaweza kuwa chanzo cha ujuzi, mitandao ya biashara, na uwekezaji wa kimataifa.

Kama hali ya sasa ya wananchi kukimbia nchi yao haitadhibitiwa, New Zealand inaweza kupoteza zaidi ya nguvu kazi yenye ujuzi, kushuka kwa uzalishaji, na kupungua kwa ukuaji wa uchumi, jambo linaloashiria changamoto kubwa za kijamii na kiuchumi kwa vizazi vijavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *