Dar es Salaam. Mama wa msanii wa Hip-hop nchini, Rashid Abdallah (Chid Benz), Hawa Idd Mwamanda amefariki dunia nyumbani kwake, usiku wa kuamkia leo Feb 11, 2025.

Akizungumza na Mwananchi, Chid Benz kwa masikitiko makubwa amethibitisha taarifa hiyo na kusema msiba kwa sasa upo nyumbani kwa mama yake, Chanika.

Hatahivyo Chid amesema taarifa kuhusu taratibu za mazishi zitatolewa familia ikijadiliana. 

“Msiba upo nyumbani kwa marehemu, mtaa wa Masantula, Chanika. Kuhusu taratibu za mazishi mimi mwenyewe nilikuwa nipo studio. Hapa ndio tunaelekea huko kama dakika kadhaa nitafika. Watu wengi wanaoniuliza nashindwa kujibu kwasababu mimi nina kaka yangu mkubwa mpaka sasa yeye aseme ndio niwafahamishe.

“Lakini bora watu wawepo ili kama taarifa itasema tunazika leo tujumuike pamoja. Kaka yangu namjua ni Shekh kwahiyo ngoja nikamsikilize,” amesema Chid.

Tunatoa pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amen.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *