
Marekani inapanga kutuma wanajeshi takriban 200 nchini Nigeria kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo katika kupambana na wanamgambo wa Kiislamu, afisa mmoja wa Marekani amesema siku ya Jumanne, wiki kadhaa baada ya Rais Donald Trump kuamuru mashambulizi ya anga dhidi ya kile alichokiita malengo ya Islamic State.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la Marekani lilitangaza wiki iliyopita kwamba lingetuma kikosi kidogo cha wanajeshi nchini Nigeria, bila kutaja idadi hiyo. Huu ni uthibitisho wa kwanza rasmi wa uwepo wa jeshi la Marekani nchini Nigeria tangu mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Washington siku ya Krismasi.
Trump amebainisha kwamba shughuli zaidi za kijeshi za Marekani zinaweza kufanyika nchini Nigeria, na shirika la habari la habari la Reuters limeripoti kwamba Marekani imekuwa ikiendesha safari za ndege za ufuatiliaji nchini humo kutoka Ghana tangu angalau mwishoni mwa mwezi Novemba.
Afisa huyo alibainisha kuwa wanajeshi hawa 200 wataimarisha kikosi cha Marekani ambacho tayari kipo nchini Nigeria ili kusaidia vikosi vya Nigeria.
Kamandi ya jeshi la Marekani Afrika (AFRICOM) haikujibu mara moja kuhusiana na madai hayo.
Nigeria iko chini ya shinikizo kubwa kutoka Washington kuchukua hatua kufuatia shutuma za Trump kwamba taifa hilo la Afrika Magharibi linashindwa kuwalinda Wakristo dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu wanaoendesha harakati zao kaskazini magharibi mwa nchi.
Serikali ya Nigeria inakanusha mateso yoyote ya kimfumo dhidi ya Wakristo, ikisema inawalenga wapiganaji wa Kiislamu na makundi mengine yenye silaha ambayo yanashambulia na kuwaua Wakristo na Waislamu.
Wapiganaji kutoka Boko Haram na Islamic State Afrika Magharibi (ISWAP) wameongeza mashambulizi yao dhidi ya misafara ya kijeshi na raia, na kaskazini magharibi bado ni kitovu cha uasi wa Kiislamu tangu miaka 17 iliyopita.
Idadi ya watu wa Nigeria zaidi ya milioni 230 imegawanywa kwa usawa kati ya Wakristo, ambao ndio wengi kusini, na Waislamu, ambao ndio wengi kaskazini.