MKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Geita kutenga fungu maalum la uwezeshaji wa vijana kutoka Fedha za Uwezeshaji wa Makampuni kwa Jamii (CSR).

Shigella ametoa maelekezo hayo katika kongamano la vijana Kujadili fursa za kiuchumi mjini Geita lililoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita na kukutanisha makundi tofauti ya vijana.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati.

Amesema wilaya ya Geita inapokea sh bilioni 9 ya CSR kwa mwaka kutoka Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu ya Geita (GGML) hiVvo mipango inapaswa kufanyika na kupata bajeti maalum ya vijana.

Ameelekeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Geita kupitia baraza la madiwani, kujadili na kupitisha fungu la makundi yote maalum kutoka CSR.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Muyenzi.

“Tuangalie ni asilimia ngapi kutoka CSR tunaipeleka kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwa ajili ya uwezeshaji kiuchumi”, amesema na kuongeza;

‘Katika zile fedha hatukatai kujenga madarasa, hatukatai kujenga vituo vya afya, hatukatai kujenga Barabara, tunahitaji CSR izalishe ajira kwa vijana wetu”.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba.

Ameongeza pia Manispaa ya Geita kwa kushirikiana na GGML wanayo nafasi ya kungalia sekta za uzalishaji maalum kwa vijana ili waweze kupewa kandarasi za kuhudumu kadri ya mitaji yao.

Shigella ameagiza kila halmashauri ihakikishe inafanya kongamano la vijana wa makundi yote na kufanya majadiliano ya kina juu ya mahitaji ya vijana na kuja na maazimio na mpango kazi.

Washiriki wa kongamano la vijana Manispaa ya Geita.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati amesema mpango wa makongamano ya vijana ni utekelezaji kwa vitendo wa sera za vijana chini ya Wizara ya Maendeleo ya Vijana.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba amesema kongamano hilo lililenga kuwajengea uwezo vijana juu ya fursa za kiuchumi na kuandaa mikakati ya uwezeshaji wa vijana kwenye sekta zote.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Muyenzi amesema azma ya kongamano la vijana ilikuwa ni kuwaleta vijana pamoja, kubainisha fursa za uwekezaji na kuwajengea uwezo vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *