Chanzo cha picha, Reuters/Getty
Rais wa Marekani Donald Trump amesema katika mahojiano na Fox News kwamba makubaliano yoyote na Iran lazima yajumuishe mpango wa makombora wa Tehran pamoja na mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.
Bw. Trump, ambaye Jumanne pia alizungumza kuhusu uwezekano wa kutuma meli nyingine kwenye Ghuba ya Uajemi, alifafanua katika mahojiano na Fax News kwamba: “Watu wengi wanasema hapana, lakini nasema ningependelea kufanya makubaliano; bila shaka lazima uwe mpango mzuri.
Hakuna silaha za nyuklia, hakuna makombora, hakuna hili na hakuna vile; kila kitu unachotaka. Lakini wengine wana wasiwasi kwa sababu, kama wanavyosema Iran, Hawakuchukua hatua miaka mingi .”
Matamshi ya Bw.Trump kuhusu maudhui ya mazungumzo na Iran yanakuja wakati ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araqchi na viongozi wengine wa Iran wanasema kwamba mpango wa makombora wa nchi hiyo “hauwezi kujadiliwa” na kwamba nchi hiyo haitaacha haki yake ya kurutubisha madini ya uranium, lakini inaweza kusitisha au kupunguza kwa muda ili kujenga imani.
Jana, J.D. Vance, makamu wa rais wa Bw. Trump alisema mjini Yerevan kwamba suala la kukandamizwa kwa umwagaji damu maandamano ya Januari nchini Iran pia liliibuliwa katika mazungumzo kati ya Tehran na Washington.