BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limewataka viongozi wapya wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) kuwa wabunifu ili kukuza vipaji vya vijana na kurejesha heshima ya mchezo huo nchini.

Akizungumza leo Februari 11, 2026, katika hafla ya makabidhiano ya vifaa iliyofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Afisa Michezo wa BMT, Apansia Lema, amesema viongozi hao wana jukumu la kuinua kiwango cha netiboli kwa kuhamasisha ushiriki wa wasichana na kuibua vipaji mikoani kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania kimataifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa CHANETA, Stella Mwangomale ameahidi kushirikiana na viongozi wenzake kuimarisha mchezo huo huku aliyekuwa mwenyekiti, Dk. Devotha Marwa akiwataka kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ili netiboli iendelee kuitangaza  Tanzania. SOMA: BMT kuzifanyia tathimini kamati za mikoa 12

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *