Zoezi la uandikishaji wa bima ya afya kwa wote kwa kaya masikini limeanza rasmi katika kata ya Genge Halmashauri ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Ayoub Sebabili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo, Ayoub Sebabili amesema kuwa wamu ya kwanza inalenga kuandikisha kaya masikini, ambapo walengwa watasajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya bima ya afya vitakavyowawezesha kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka mzima.
Pia amewataka Wananchi kufuata maelekezo yalitolewa na kutoa onyo kwa yeyote atakae tumia bima ya mtu mwingine ili kupata matibabu Ikiwa ni kinyume Cha taratibu na sheria zilizowekwa
Nao wakazi wa wilaya hiyo wameishukuru Serikali kwa kutoa Bima ya bure kwa Wananchi
Katika Wilaya ya Muheza wakazi 4886 wanatarajiwa kunufaika na bima ya afya bure Kwa wote.
(Feed generated with FetchRSS)