• Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, ametangaza vita dhidi ya uongozi wa ODM kufuatia kuondolewa kwa seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, katika kiti cha katibu mkuu wa chama
  • Babu aliwashutumu maafisa wakuu wa ODM, akiwemo seneta wa Siaya Oburu Oginga, kwa kukiuka kiapo chao na kufanya “mkutano wa kiholela” Mombasa ili kumbandua Sifuna
  • Mbunge huyo mwenye kauli kali aliwataka wanasiasa wengine ndani ya ODM watangaze msimamo wao, akionya kuwa mapambano hayo hayatamalizika hivi karibuni
  • Babu alitetea rekodi ya Sifuna, akisema kuwa “makosa” yake pekee ni kupigania wanyonge, na akaeleza kuondolewa kwake kama shambulizi la kisiasa

Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, alitoa onyo kali kwa maafisa wakuu wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM).

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino
Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino alitoa onyo kwa uongozi wa chama cha ODM, akisema kuwa vita hivyo vitakuwa vya muda mrefu. Picha: Babu Owino.
Source: Twitter

Hii inafuatia kuondolewa kwa seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, kama katibu mkuu wa chama, huku Babu akieleza hatua hiyo kama mstari mwekundu na ishara kwamba vita ya kuokoa roho ya chama imeanza.

Pia soma

Catherine Omanyo: Wasifu wa Mbunge Aliyeteuliwa Kuwa Katibu Mkuu wa ODM baada Sifuna Kuondolewa

Kwa nini Babu Owino alitoa onyo kwa maafisa wa ODM?

Katika mkutano na wanahabari uliojaa hisia kali Alhamisi, Februari 12, Babu alionyesha kuwa mapambano ya haki na kulinda misingi ya chama hayawezi kujadiliwa.

Mwanasiasa huyo kijana aliwataka viongozi wengine wa ODM watangaze wazi upande wao, akitangaza kuwa mapambano yameanza rasmi.

“Asanteni mabibi na mabwana. Nataka kuwahakikishia kwamba tutapigana. Vita vimetangazwa, mstari umechorwa. Kama uko upande wetu, uko upande wetu. Kama uko upande wa pili, pigana huko, lakini hili halitaisha hivi karibuni,” Babu alitangaza.

Kwa nini Babu alisema kuondolewa kwa Sifuna ni batili?

Babu alipuuza uamuzi wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Taifa (NEC) kumuondoa Sifuna, akieleza kuwa ni kinyume cha sheria, na akashangaa jinsi “uongozi ulioundwa kinyume cha sheria” unaweza kumuondoa kiongozi aliye madarakani kihalali.

Alimshutumu kiongozi wa ODM na seneta wa Siaya, Oburu Oginga, kwa kukiuka kiapo alichokula wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya chama.

Aidha, alidai kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu, akisisitiza kuwa waliokula kiapo kitakatifu cha kulinda katiba ya chama ndio waliokiuka katiba hiyo.

Pia soma

Edwin Sifuna Aashiria Ataenda Mahakamani Kupinga Hatua ya ODM Kumbandua: “Mimi Bado ni Katibu Mkuu”

“Nataka kusema kwamba kuondolewa kwa Sifuna madarakani kinyume cha sheria hakuchukuliwi kwa mzaha na timu hii, na ninawalaani viongozi waliofanya hivi. Tunajua Baba alisimamia nini alisimamia haki, alisimamia kusikilizwa kwa haki na kesi ya haki. Mkutano uliofanyika Mombasa ulikuwa haramu. Ulikuwa mkutano wa kiholela uliopangwa kumuondoa katibu mkuu wa sasa wa ODM, Edwin Sifuna, madarakani,” Babu alisema.

Edwin Sifuna
Babu Owino alidai Sifuna alifurushwa kwa sababu ya kusimama na Wakenya. Picha: Edwin Sifuna.
Source: Facebook

Mbunge huyo alidai kuwa baadhi ya viongozi wamepewa jina la waasi ndani ya ODM kwa sababu ya kusimama na Wakenya wa kawaida.

Kulingana na mbunge huyo wa Embakasi, hii ndiyo chanzo cha matatizo ya seneta huyo wa Nairobi ndani ya chama.

Mwisho, nataka kusema kwamba kosa pekee alilofanya Sifuna, na makosa pekee tunayofanya sisi, ni kupigania wanyonge, kupigania waliosahaulika katika jamii hii, kupigania wasiojiweza nchini Kenya, kupigania ajira kwa vijana wetu, na kupinga gharama ya juu ya maisha inayowaathiri Wakenya katika taifa hili. Hayo ndiyo makosa pekee tunayofanya,” Babu aliongeza.

Sifuna aapa kujipigania kufuatia kuondolewa kwa katika ODM

Hapo awali, seneta huyo wa Nairobi aliyekumbwa na mvutano alisisitiza kuwa hatajiuzulu licha ya NEC ya chama kuamua kumuondoa.

Alieleza uongozi wa Oburu kuwa batili na kudai kuwa wadhamini wa chama walizuiwa kuendeleza mazungumzo ya maridhiano.

Sifuna aliapa kupinga uamuzi wa NEC kupitia njia zote za kisheria, akisisitiza dhamira yake ya kulinda misingi ya ODM na urithi wa Raila Odinga.

Pia soma

Video ya William Ruto akiahidi kumwadhibu Edwin Sifuna yaibuka tena baada ya kuondolewa kwake

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *