
Kaimu mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) ametua mnamo Februari 12, 2026, katika Uwanja wa Ndege wa Goma, ambao ulikuwa umefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ziara hii ni sehemu ya maandalizi ya kuunga mkono “Mfumo wa Ufuatiliaji na Uthibitishaji wa Usitishaji Mapigano” mashariki mwa Kongo, kama ilivyoainishwa na Mkataba wa Doha. Muhimu zaidi, inaashiria kufunguliwa tena kwa uwanja huu wa ndege wa kimataifa, ambao umefungwa tangu mji huo ulipotekwa na kundi la kisiasa na kijeshi la AFC/M23.
Kutua kwa ishara kubwa kulifanyika Alhamisi asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Kaimu mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO), Vivian van de Perre, aliwasili Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, mji ulio chini ya udhibiti wa kundi la kisiasa-kijeshi la AFC/M23 linaloungwa mkono na Rwanda kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Helikopta ya MONUSCO ilitua muda mfupi kabla ya saa sita mchana, kwa saa za Mashriki mwa DRC, katika uwanja wa ndege wa Goma, ambao umefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na mapigano makali kati ya jeshi la Kongo na waasi wa AFC/M23.
Vivian van de Perre amekumbusha jambo hili alipofika. “Nilikuwa kwenye ndege ya mwisho kutua Goma, mnamo Januari 26, 2025,” amewaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Goma. “Leo, niko kwenye helikopta ya kwanza kutua huko tena, na natumai hii itakuwa mwanzo wa kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege kwa manufaa ya watu,” ameongeza.
Kuanza tena kwa safari za ndege za Umoja wa Mataifa
Kutua huku kunamaanisha, kwa upande mmoja, kwamba MONUSCO inarejesha udhibiti wa kituo chake – ambacho kitaruhusu kuanza tena kwa safari za ndege za Umoja wa Mataifa na safari za ndege zinazoweza kuwa za kibinadamu – na kwa upande mwingine, kwamba Umoja wa Mataifa karibu umepata dhamana za usalama kutoka kwa AFC/M23. Dhamana hizi ziliombwa siku chache zilizopita na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, ili kutumia uwanja wa ndege kwa ajili ya misheni za upelelezi wa angani kabla ya kupelekwa kwa walinda amani Uvira, katika mkao jirani wa Kivu Kusini.
Vivian van de Perre amebainisha mnamo Februari 12, 2026, kwamba MONUSCO itapeleka ujumbe wake wa kwanza wa upelelezi wa angani Uvira katika siku zijazo. Ameongeza kuwa ziara yake inalenga kushirikiana na wadau husika ili kuendeleza maandalizi ya Mfumo wa Ufuatiliaji wa Usitishaji Mapigano kufanya kazi kwa uaminifu.
Walinda amani 8,000 Mashariki
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC – ambao una walinda amani 8,000 mashariki mwa nchi – umedumisha kambi zake huko Goma baada ya jiji hilo kutekwa lakini haukuwa na ufikiaji tena wa uwanja wa ndege.
Mashariki mwa Kongo, eneo lenye utajiri wa maliasili na linalopakana na Rwanda, limekuwa likikumbwa na vurugu kwa miaka 30. Makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano na mapatano ya amani yamesainiwa tangu mwishoni mwa mwaka 2021 na kuibuka tena kwa kundi lenye silaha la M23 linaloungwa mkono na Rwanda katika eneo hilo. Mapema mwaka wa 2025, AFC/M23 na washirika wake waliteka miji mikubwa ya Goma na Bukavu mfululizo kufuatia shambulio.
Makubaliano mawili yamesainiwa tangu wakati huo: tamko la kanuni huko Doha na AFC/M23 na serikali ya Kinshasa, likielezea ahadi za kusitisha mapigano, na makubaliano “ya amani na ustawi,” yaliyoidhinishwa mwezi Desemba huko Washington na DRC na Rwanda. Hadi sasa, hakuna hata moja ya makubaliano haya ambayo yamemaliza mapigano.