Libya imetoa leseni kwa ajili ya uchimbaji na uzalishaji mafuta kwa makampuni kadhaa za nishati za kigeni, ikiwa ni pamoja na makampuni makubwa ya Chevron na BP kwa mara ya kwanza tangu kupinduliwa mamlakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.

Sekta ya mafuta ya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini imepitia katika changamoto kubwa kufuatia uasi uliomng’oa madarakani na Gaddafi mwaka wa 2011.

Hata hivyo, Lakini kutokana na uzalishaji na mauzo ya nje ya nishati kuwa na nguvu zaidi tangu wakati huo, Libya sasa imejikita katika kuyavuta nchini makampuni makubwa ya nishati duniani.

Mbali na Kampuni ya Chevron, makampuni ya nje yaliyoshinda jana  wakati wa raundi ya hivi karibuni ya zabuni ni pamoja na kampuni kubwa zaidi ya nishati  ya sekta binafsi ya barani Afrika, kwa jina la  Aiteo ya nchini Nigeria.

Wazabuni wengine walioshinda walikuwa ni :Kampuni ya  Repsol ya Uhispania pamoja na  BP, Eni ya Kaskazini mwa Afrika inayoshirikiana na  QatarEnergy n.k.

Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Libya (NOC) haikuweka wazi gharama ya leseni hizo na kwamba kutakuwa na duru nyingine ya zabuni baadaye mwaka huu.

Libya kwa sasa inazalisha takriban mapipa milioni 1.5 kwa siku, huku ikiwa ni akiba kubwa zaidi ya mafuta barani Afrika inayokadiriwa kuwa mapipa bilioni 48.4.

Mwezi uliopita Libya ilisaini makubaliano ya thamani ya dola bilioni 20 ya uwekezaji wa makampuni ya TotalEnergies na ConocoPhillips kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mafuta kwa zaidi ya miaka 25. 

Mamlaka husika za Libya zimesema kuwa lengo nikuongeza uzalishaji wa mafuta kila siku kwa mapipa 850,000 ndani ya muda huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *