Zaidi ya watu 30 wamefariki baada ya Kimbunga Gezani kupiga Madagasar kwa kasi kubwa siku ya Jumanne, na kuacha angalau theluthi mbili ya jiji la pili kwa ukubwa la kisiwa cha Toamasina kuwa magofu, maafisa wamesema.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kimbunga hicho kilichojaa upepo mkali kiliua watu wasiopungua 31 kilipopiga Madagasar, na kuangusha nyumba na kusababisha mafuriko makubwa, mamlaka ya maafa ya kisiwa cha Bahari ya Hindi kilisema siku ya Jumatano.

Kimbunga Gezani kilitua Jumanne, kikipiga jiji la pili kwa ukubwa nchini, Toamasina, huku upepo ukifikia kilomita 250 kwa saa.

Ofisi ya Kitaifa ya Usimamizi wa Hatari na Maafa (BNRGC) ilisema kwamba wengi walifariki baada ya nyumba zao kuwaangukia.

Gezani pia iliwaheruhi vibaya angalau watu 36. Zaidi ya wakazi 2,740 walihamishwa kama tahadhari baada ya kimbunga hicho kupiga jamii za pwani kabla ya kuhamia ndani ya nchi.

Matokeo ya kimbunga hicho yaliwaacha watu wengine 6,870 bila makaazi, huku jumla ya watu 250,406 wakiorodheshwa kama waathiriwa wa maafa, BNGRC imesema.

“Kilichotokea ni janga: karibu asilimia 75 ya jiji la Toamasina liliharibiwa,” amesema kiongozi mpya wa nchi hiyo, Kanali Michael Randrianirina, ambaye alizuru Toamasina kabla ya kutua kwa kimbunga hicho ili kuwasaidia wakazi.

“Hali ya sasa inazidi uwezo wa Madagascar pekee,” alisema Randrianirina, ambaye alichukua madaraka mwezi Oktoba, akitoa wito kwa “washirika wa kimataifa na wafadhili” kusaidia kisiwa hicho maskini.

(RFI pamoja na AFP, Reuters)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *