Mamia ya Waturuki wamejitokeza leo Alhamisi Februari 12, 2026 kwenye mazishi ya muigizaji, Kanbolat Görkem maarufu kwa uhusika wake kama Savci Bey kwenye tamthilia ya OTTOMAN, yaliyofanyika kwenye makaburi ya Zincirlikuyu jijini Istanbul.

Kwa mujibu wa mwandaaji wa tamthilia hiyo, Mehmet Bozdağ, Kanbolat amefariki kufuatia maradhi ya moyo licha ya kuugua ghafla Jumanne wiki hii na kukimbizwa hospitali, ambako umauti ulimfika.

Amezaliwa Novemba 4, 1980 mjini Düzce Uturuki, ni msomi wa masuala ya filamu kutoka Chuo Kikuu Cha Theatre Department at Hacettepe. Alianza safari yake ya sanaa mwaka 2004 aliposhiriki kwenye tamthilia maarufu ya Çemberimde Gül Oya.

#Savcibey #KanbolatGörkem

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *