
Dar es Salaam. Taarifa ya mshitakiwa wa uhaini, Tundu Lissu mbele ya mahakama kwamba hajala, imewalazimu jopo la majaji wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, kuahirisha kesi hiyo hadi kesho.
Baada ya majaji kutoka katika ukumbi wa Mahakama ya wazi namba moja inamosikilizwa kesi hiyo vilio na makelele ya lawama kutoka kwa ndugu, wanachama na wafuasi wa Chadema waliokuwamo mahakamani ndipo vikalipuka hususan kwa wanawake, huku wanaume kila mmoja akitamka neno lake mradi tu kupinga na kulaani jambo hilo.
Hali hiyo imefanya ukumbi wa mahakama hiyo kutawaliwa na makelele ya vilio hivyo na maneno hayo ya lawama dhidi ya Jeshi la Magereza na Serikali kwa ujumla, kwa madai ya kiongozi huyo kuonewa kutokana na namna anavyotendewa.
Vilio hivyo vilitokana na taarifa ya Lissu kuwa hajala tangu afikishwe mahakamani hapo asubuhi, lakini alisema yuko tayari kuendelea na kesi.
Kutokana na taarifa hiyo baada ya Mahakama kushauriana na pande zote ikaahirisha kesi hiyo kwa kuda wa dakika 15 huku ikielekeza mshtakiwa Lissu apatiwe chakula, lakini hata baada ya kurejea Lissu akaijulisha tena mahakama kuwa bado alikuwa hajapata chakula.
Ingawa yeye alipendekeza kuendelea na usikilizwaji hata katika mazingira hayo ya kutokula, lakini Mahakama imesema suala la afya ni haki ya msingi kwa mshtakiwa kama ilivyo kwa jaji na watu wengi na kwamba katika hiyo haiwezi kuendelea na kesi hiyo ndipo ikaiahirisha mpaka kesho saa 3:00 asubuhi.
Kutokana na taarifa hiyo ya Lissu, kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo, Dunstan Nfunguru ameuliza utaratibu wa chakula chake na Lissu akajibu kuwa suala la chakula cha wafungwa mahabusu liko katika mamlaka ya Jeshi la Magereza.
“Magereza wana pesa zangu nyingi tu wanatunza wao na huwa wanakata kwa huduma ya chakula. Lakini leo sijala. Nimelazimika kulisema hili kuwapeni taarifa hiyo maana nisipolisema mimi hakuna mwingine wa kusema,” amesema Lissu na kusisitiza kuwa yuko tayari kuendelea na kesi.
Ilivyokuwa
Lissu amefikishwa mahakamani hapo kutoka mahabusu katika Gereza la Ukonga anakohifadhiwa saa 2:55 na kupelekwa katika mahabusu ya Mahakama kusubiri muda wa kupanda kizimbani.
Saa 3: 40 alipandishwa kizimbani na kesi ikaanza kwa shahidi wa nne wa Jamhuri mpaka saa 6:20 mchana shahidi huyo alipomaliza ushahidi wake.
Baada ya shahidi huyo wa nne kumaliza upande wa mashtaka uliomba ahirisho la muda mpaka saa 8 mchana kumsubiri shahidi wake wa tano na mahakama ikakubaliana na ombi hilo.
Baada ya kurejea upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa shahidi wao alikuwa tayari ameshafika na kwamba wako tayari kuendelea.
Lissu alipoulizwa na mahakama kama alikuwa tayari ndipo akaitaarifu kuwa yuko tayari kuendelea ingawa hajala.
Kutokana na taarifa hiyo baada ya mahakama kushauriana na pande zote ikaahirisha kesi hiyo kwa kuda wa dakika 15 huku ikielekeza mshtakiwa Lissu apatiwe chakula, lakini hata baada ya kurejea Lissu akaijulisha tena mahakama kuwa bado alikuwa hajapata chakula.
Ingawa yeye alipendekeza kuendelea na usikilizwaji hata katika mazingira hayo ya kutokula, lakini mahakama imesema kiwa suala la afya ni haki ya msingi kwa mshtakiwa kama ilivyo kwa jaji na watu wengi na kwamba katika hiyo haiwezi kuendelea na kesi hiyo ndipo ikaahirisha mpaka kesho saa 3:00 asubuhi.
Kutokana na taarifa hiyo ya Lissu kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo, Dunstan Nfunguru ameuliza utaratibu wa chakula chake na Lissu akajibu kuwa suala la chakula cha wafungwa mahabusu liko katika mamlaka ya Jeshi la Magereza.
“Magereza wana pesa zangu nyingi tu wanatunza wao na huwa wanakata kwa huduma ya chakula. Lakini leo sijala. Nimelazimika kulisema hili kuwapeni taarifa hiyo maana nisipolisema mimi hakuna mwingine wa kusema,” amesema Lissu na kusisitiza kuwa yuko tayari kuendelea na kesi.
Hata hivyo, baada ya majaji wanaoisikiliza kesi hiyo kujadiliana kwa muda wakaamua kuahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 15 na kuelekeza ufanyike utaratibu wa kumpatia mshtakiwa huyo chakula chochote kabla ya kuendelea.
Lissu amekubaliana nao kuahirisha kwa muda apate chochote kinachoweza kupatikana kisha waendelee, lakini si kuahirisha mpaka kesho.
Baada ya muda huo wa ahirisho fupi kuisha na mahakama ikarejea tena Lissu ameitaarifu mahakama kuwa bado alikuwa hajala, jambo ambalo limeilazimu mahakama kusimamisha kuendelea na usikilizaji wa kesi hiyo na badala yake ikaiajirisha mpaka kesho.
Suala hilo limelifanya Jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo kujadiliana kwa muda na kufikia uamuzi wa kuiahirisha moja kwa moja kesi hiyo mpaka kesho.
“Kabla ya kuahirisha kwa muda shauri hili tumezungumza na tumeelekeza kuwa suala la afya ni haki ya msingi kwa kila mtu iwe mshtakiwa hata kwa jaji.” amesema Jaji Ndunguru.
Amesema kuwa kwa kuzingatia hali hii hawawezi kuendelea na shauri hili wakati mshtakiwa hajala hii ni kinyime na haki za binadamu na kwamba mahakama ina wajibu wa kulisimamia .
“Kwa hiyo tunaahirisha mpaka kesho saa 3:00 asubuhi,” amesema Jaji Ndunguru na kuagiza kwa mamlaka yenye dhamana ya chakula cha mshtakiwa huyo kuweka utaratibu kuhakikisha kuwa anakuwa anapatiwa huduma hiyo.
Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kusudio la kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Anadaiwa kuwa Aprili 3, 2025, jijini Dar es Salaam, akiwa raia wa Tanzania, kwa nia ya uchochezi alishawishi umma kuzuia kufanyia kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, huku akitamka na kuandika maneno ya kumshinikiza kiongozi Mkuu wa Serikali ya Tanzania kuwa,
“Wakisema msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli…, kwa sababu tunasema tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi, hivyo ndivyo namna ya kupata mabadiliko…, kwa hiyo tunaenda kikinukisha…, sana sana huu uchaguzi tutaenda kuuvuruga kwelikweli…, tunaenda kukinukisha vibaya sana…”
Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Iringa, Dunstan Ndunguru akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka.
Mpaka sasa jumla ya mashahidi wanne kati ya 30 wa Jamhuri wameshatoa ushahidi wao.