Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa hii leo kwenye wavuti wa OCHA, huu ni mlipuko mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini DRC katika kipindi cha takribani miaka 25. Tangu mwanzoni wa mwaka huu, zaidi ya wagonjwa 1,300 wamegundulika kuugua kipindupindu huku vifo 35 vikiripotiwa.

Upungufu ni mkubwa

Serikali ya DRC, Umoja wa Mataifa na washirika wao wanaendelea kutoa msaada, hata hivyo bado kuna mapungufu makubwa. Huduma za maji, usafi wa mazingira na afya zina uhaba mkubwa wa fedha, wahudumu wa afya wameelemewa na kazi, vifaa vinaendelea kupungua, na upatikanaji wa vituo vya matibabu bado ni changamoto.

Katika kukabiliana na upungufu huo 

Siku ya Jumatatu, dola za Marekani Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetenga dola 750,000 ili kuwasaidia wadau wa masuala ya kibinadamu wanaofanya kazi katika sekta ya afya ili waweze kupanua kwa haraka huduma za kuokoa maisha na kudhibiti kasi ya maambukizi.

Hii ni mara ya nne tangu mapema mwaka 2025 kwa CERF kutoa fedha kwa ajili ya kile kinachoitwa hatua za tahadhari, hatua inayolenga kuchukua hatua mapema kabla ya majanga yanayotabirika kuongezeka na hivyo kuokoa maisha zaidi. 

Mwaka jana, DRC ilirekodi zaidi ya wagonjwa 71,800 wa kipindupindu na zaidi ya vifo 2,000.

Umoja wa Mataifa na washirika wake wanahitaji kwa dharura ufadhili zaidi na ulio rahisi kutumika ili kuimarisha huduma za afya, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kutosha, pamoja na kufuatilia maeneo yaliyoathiriwa na kipindupindu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *