
Wabunge kadhaa wa chama cha Republican kutoka Baraza la Wawakilishi la Marekani wamepinga Donald Trump siku ya Jumatano na kupiga kura ya kufuta ushuru kwa Canada, jambo ambalo pigo kubwa kwa rais wa Marekani ambaye amewatishia wawakilishi waliopinga wakati wa upigaji kura.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Muswada huo sasa utawasilishwa kwa Baraza la Seneti kwa ajili ya upigaji kura. Lakini hata kama utapitishwa, utapigwa kura ya turufu na rais wa Marekani, ambaye amefanya ushuru kuwa msingi wa sera yake ya kiuchumi.
Kura mpya tu katika Bunge na kupitishwa kwa wingi wa theluthi mbili ndio kutabadilisha kura hii ya turufu, jambo ambalo huenda lisiwezekani kutokana na wingi wa wabunge kutoka chama cha Republican unaoshikiliwa katika mabunge yote mawili. Kwa hivyo azimio hilo ni la kiishara.
Wakati wa upigaji kura, Donald Trump alionya kwamba wanachama wa chama chake waliopiga kura dhidi ya ushuru wake “watakabiliwa na hatua kubwa wakati wa uchaguzi, ikiwa ni pamoja na katika kura za mchujo.” “Ushuru umetupa usalama wa kiuchumi na kitaifa, na hakuna mrepublican anayepaswa kuwajibika kwa kuharibu fursa hiyo,” ameongeza katika ujumbe kwenye jukwaa lake la Truth Social.
“Ushuru ni kodi kwa watumiaji wa Marekani”
Licha ya haya, wanachama sita wa chama kilicho na idadi kubwa ya wabunge na maseneta walijiunga na Chama cha Democratic kukomesha hali ya hatari iliyotangazwa na rais mnamo mwezi Februari 2025, ambayo ilimuwezesha kutoza ushuru kwa bidhaa zilizoagizwa kutoka Canada.
Kura hiyo ilikuja baada ya kumalizika kwa hatua iliyopiga marufuku kupiga kura yoyote kuhusu suala la ushuru. Kiongozi wa Chama cha Republican, Mike Johnson, alijaribu hadi Jumanne jioni kuongeza muda huo, lakini bila mafanikio.
Watetezi wa biashara huria, maafisa wengi waliochaguliwa wa mrengo wa kulia wanapinga hadharani sera za ulinzi za Donald Trump, hasa kwa kuwa ni Bunge, si rais, ambalo lina mamlaka ya kikatiba ya kutoza ushuru.
Akithibitisha tena haki hii ya kisheria, mbunge wa Chama cha Republican, Don Bacon alisema siku ya Jumatano: “Hatuwezi na hatupaswi kutoa majukumu yetu nje.” “Kama mhafidhina wa zamani, najua kwamba ushuru ni kodi kwa watumiaji wa Marekani,” alitangaza kwenyemtadao wa kijamii wa X kabla ya kupiga kura ya kuyafuta ushuru huo.