
Viongozi wa nchi mbalimbali wametuma jumbe kwa Rais wa Iran wakimpongeza kwa mnasaba wa Siku ya Taifa ya Iran na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Jana Jumatano, Februari 11 mwaka ilisadifiana na tarehe 22 mwezi Bahman mwaka 1404 Hijria Shamsia kwa mujibu wa kalenda ya Iran ambayo ni siku ya maadhimisho ya kutimia mwaka wa 47 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Mamilioni ya wananchi kutoka matabaka yote ya kijamii walijitokeza mitaani kote nchini Iran kushiriki maandamano ya kitaifa ya maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Viongozi wa mataifa mbalimbali wametuma salamu za pongezi kwa serikali na wananchi wa Iran kwa mnasaba wa maadhimisho haya.
Katika ujumbe wake wa pongezi kwa Rais, serikali, na watu wa Iran kwa maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Rais wa China Xi Jinping alisema: “China na Iran ni marafiki wazuri na washirika wazuri, na ninaona umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Iran.”
Mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud na mrithi wa kiti cha ufalme wan chi hiyo Muhammad bin Salman wametoa salamu za pongezi kwa nyakati tofauti na kuwapongeza wananchi wa Iran na serikali kwa maadhimisho haya.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, ikichapisha picha ya bendera ya nchi hiyo kando ya bendera ya Iran kwenye X-Net, iliandika: “Tunaipongeza kwa dhati nchi jirani yetu Iran, kwa kusherehekea Siku yake ya Kitaifa.
Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amemtumia ujumbe Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, akimpongeza maadhimisho ya Siku ya Taifa ya Iran na ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Katika ujumbe wake rasmi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amempongeza Rais na watu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo na ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto za kimataifa.
Baadhi ya viongozi wengine waliotuma ujumbe wa pongezi Waziri Mkuuu wa Pakistan, TRais wa Azerbaijan na Waziri wa Mambo ya Nje wa India.