Katika “Biashara ya kukata tamaa,” kundi la uchunguzi la All Eyes on Wagner linachunguza mitandao inayowaajiri wapiganaji wa Kiafrika kwa ajili ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya kwanza, kundi hilo linachapisha orodha ya waajiriwa na wale waliouawa kwenye mstari wa mbele, ili kusaidia familia ambazo hazia taarifa yoyote kuhusu wapendwa wao.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanathibitshwa na Linda ambaye sasa amekata tamaa. Tangu mwezi Julai 2024, hajapata habari zozote kuhusu mumewe, ambaye aliondoka wiki chache zilizopita kwenda Urusi akiwa na ahadi ya kazi yenye malipo mazuri, ya kutosha kutuma pesa kwa wazazi wake wagonjwa na mtoto wao wa miezi miwili. Linda alisimulia mateso yake na uchungu wake kwenye RFI mwaka jana.

Asubuhi ya leo mnamo Februari 2026, anapata taarifa kwamba jina la Joel linaonekana kwenye orodha ya waajiriwa wa Kiafrika waliouawa nchini Ukraine. Aliunganishwa kwenye kikosi cha 255 cha nchi kavu. Kifo chake kilirekodiwa rasmi Mei 24, 2025, miezi kumi baada ya kutoweka kwake. Alikuwa na umri wa miaka 24. Linda anauliza kilichotokea kwa mwili wake, kama alizikwa, kama kuna angalau kaburi. Ni vigumu kumjibu.

Orodha hii ilichapishwa siku ya Jumatano Februari 11 katika ripoti mpya ya kundi la uchunguzi la All Eyes On Wagner (AEOW). Ina majina ya wapiganaji 1,417 kutoka nchi 35 kote barani ambao waliandikishwa katika jeshi la Urusi kati ya mwaka 2023 na katikati ya mwaka 2025, 316 kati yao walifariki. Ingawa Misri ndiyo nchi inayowakilishwa zaidi miongoni mwa walioandikishwa (361), Cameroon imelipa gharama kubwa zaidi, huku vifo 94 kati ya wapiganaji 335 waliosajiliwa. Waajiriwa wa Gambia pia wamepata hasara kubwa: kati ya wapiganaji 56 walioorodheshwa baada ya kusaini mkataba, 23 walifariki. Joel, kutoka Cameroon, anahesabiwa hata miongoni mwa wanajeshi wa kikosi cha Gambia, labda kutokana na hitilafu ya kiutawala ya Urusi.

Kiwango cha vifo kinachozidi 22%

Orodha hii iliyopatikana kupitia mpango wa Ukraine wa “Nataka Kuishi”, ambao unawahimiza wapiganaji wa Urusi kujisalimisha, inatoa wazo la mauaji yanayoendelea, huku kiwango cha vifo miongoni mwa waajiriwa kikizidi 22%, bila kuhesabu waliojeruhiwa na waliotoweka. Umri wa wale walioajiriwa unaanzia miaka 18 hadi 57, huku wastani wa miaka 31 ukiongezeka. Familia nyingi kote barani Afrika zina wasiwasi, kutokana na kukosa taarfa kuhusu wapendwa wao.

Kwa Lou Osborne wa kundi la All Eyes On Wagner, anasema uchapishaji wa orodha hii unapaswa “kuruhusu familia, mara nyingi ambazo hazina taarifa yoyote kwa miezi kadhaa, kujua hatima ya wapendwa wao, kuwasiliana na mamlaka yao ya kitaifa kuomba kurejeshwa kwa mabaki na wale walionaswa, na kuchukua hatua dhidi ya uajiri huu, ambao umeongezeka kadri mashamulizi dhidi ya Ukraine yanavyoendelea.”

Katika wiki za hivi karibuni, ushuhuda kutoka kwa wapiganaji, maveterani, na familia umeongezeka. Kwa mfano, wiki iliyopita, kituo cha habari cha Marekani CNN kilirusha video, iliyotolewa na familia ya mpiganaji wa Kenya anayeitwa Francis, ambaye picha yake hivi karibuni ilisambaa sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya video kusambaa: anaonekana akiwa amefungiwa bomu, sauti ya Urusi inamwita “mfungua kopo,” kisha anasogea mbele na kuongoza kundi lake hadi kwenye handaki upande wa UKraine. Kwenye CNN, anaonya kuhusu “mauaji” nchini Urusi.

Katika ripoti ya hivi karibuni ya Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa ya Ufaransa (Ifri) kuhusu “Sera ya Urusi ya Kuajiri Wapiganaji na Wafanyakazi katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara,” mtafiti Thierry Vircoulon anakadiria kuwa kati ya wapiganaji 3,000 na 4,000 kati ya wapiganaji 18,000 hadi 20,000 wa kigeni katika safu ya jeshi la Urusi ni Waafrika.

“Tangu mwaka 2023, Urusi imeongeza juhudi zake za kuwatofautisha wanajeshi wake, kwa vita hivi,” kundi la All Eyes On Wagner linaandika. Moscow kwanza iliondoa magereza yake kabla ya kutafuta rasilimali nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na barani Afrika: “Mbali na kuwa athari mbaya, uajiri huu ndio uti wa mgongo wa mkakati uliojengwa karibu na wapiganaji ili kuingizwa katika mawimbi ya mashambulizi yanayotumika kuzidi safu za ulinzi za Ukraine.”

Kulingana na ripoti ya Ifri, kampeni za uajiri zinawalenga “vijana maskini wa mijini ambao wanaona uhamiaji wa kiuchumi kama suluhisho la maisha bora na wanaelewa kwamba Ulaya ni mahali pa kufikiwa zaidi. Kwa kuendeshwa hasa na nia za kiuchumi, wale walioajiriwa mara nyingi hudanganywa na ofa za uwongo za mafunzo na ajira. Hizi ni tabia za unyanyasaji na za kupotosha za uajiri.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *